Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,377
- 8,075
Iran inasema imeshindwa kufikia makubaliano na Saudi Arabia kuhusu mipango ya raia wake kuweza kwenda Kuhijji Makka mwezi Septemba.
Ni ishara ya hivi karibuni inayodhihirisha jinsi uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ulivyo mbaya.
Iran imerusha lawama zote kwa kushindwa kufikia makubaliano na Saudia.
Inasema Saudia ilionyesha ujeuri, na mwenendo usio sawa katika majadiliano.
Ni mazungumzo yaliofanyika katika wakati ambao sio muafaka.
Kuna mzozo mkubwa kati ya mataifa hayo mawili baada ya ibada ya hajj iliofanyika mwaka jana ambapo mamia ya raia wa Iran walifariki katika mkanayagano uliozuka.
Na baadaye uhusiano wote wa kidiplomasia ulivunjwa kutokana na hatua ya Saudi Arabia kumuua kiongozi wa madhehebu ya Shia anayetoka Iran, Nimr al-Nimr.
My Take: wale waamini mabunduki, kila siku mnapost kuhusu mabomu na mabunduki humu, ooh mara nchi fulani imetengeneza hiki mara imeuziwa bomu fulani hatari, haya sasa watumie hayo mabomu kutatua tatizo hili tuone.