Iran;Marekani ilitaka kutushambulia 2001 lakini wakashindwa

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,784
20,154
Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Marekani ilitaka kuivamia nchi hii mwaka 1991 na 2001, lakini ikashindwa kutokana na kuwa macho na uwezo wa kujihami taifa hili.
Brigedia Jenerali Ahmad Reza Pourdastan amefafanua kuwa, wakati Marekani iliingia Mashariki ya Kati kwa kuungwa mkono na nchi 30 waitifaki, lengo lake kuu halikuwa kuzivamia Iraq na Afghanistan.
Ameongeza kuwa, Washington ilitaka kuivamia Iran katika vipindi hivyo lakini ikashindwa kuthubutu kuchukua hatua hiyo kutokana na kuwa ngangari na utayarifu wa vikosi vya Iran kwa kuungwa mkono na wananchi.
Amesema vikosi vya jeshi la taifa hili vitaendelea kuwa macho na kujiandaa kwa ajili ya chokochoko zozote za adui na wavamizi wa nchi ajinabi.
Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Ahmad Reza Pourdastan amebainisha kuwa, mfumo wa kiulinzi wa Iran umejiandaa kikamilifu kujilinda.
Septemba mwaka jana, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei alisema daimaJamhuri ya Kiislamu litaendelea kusimama kidete na kuwa tayari kumkabili adui na kusisitiza kuwa, taifa hili linakabiliwa na maadui kutokana na misimamo yake katika masuala ya Uislamu, uhuru na thamani za kibinadamu.
IRIB
 
Huwa sina imani na Usa nia ya kuivamia Iran anayo anatafuta tu sababu walianzishe na sidhani kama atasita kutumia nyuklia iwapo iran ataonesha kuwa mgumu kwa silaha za kawaida
 
Dawa ya Iran ni Israel tu, na hivi soon utasikia mwanasayansi mwingine wa Iran kauliwa
 
Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, serikali ya Marekani ilitaka kuivamia nchi hii mwaka 1991 na 2001, lakini ikashindwa kutokana na kuwa macho na uwezo wa kujihami taifa hili.
Brigedia Jenerali Ahmad Reza Pourdastan amefafanua kuwa, wakati Marekani iliingia Mashariki ya Kati kwa kuungwa mkono na nchi 30 waitifaki, lengo lake kuu halikuwa kuzivamia Iraq na Afghanistan.
Ameongeza kuwa, Washington ilitaka kuivamia Iran katika vipindi hivyo lakini ikashindwa kuthubutu kuchukua hatua hiyo kutokana na kuwa ngangari na utayarifu wa vikosi vya Iran kwa kuungwa mkono na wananchi.
Amesema vikosi vya jeshi la taifa hili vitaendelea kuwa macho na kujiandaa kwa ajili ya chokochoko zozote za adui na wavamizi wa nchi ajinabi.
Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Brigedia Jenerali Ahmad Reza Pourdastan amebainisha kuwa, mfumo wa kiulinzi wa Iran umejiandaa kikamilifu kujilinda.
Septemba mwaka jana, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei alisema daimaJamhuri ya Kiislamu litaendelea kusimama kidete na kuwa tayari kumkabili adui na kusisitiza kuwa, taifa hili linakabiliwa na maadui kutokana na misimamo yake katika masuala ya Uislamu, uhuru na thamani za kibinadamu.
IRIB
Wewe Shia kila siku waleta propaganda zako za Kishia mara Kuwait ina walimu 4 wa physcs/math, mara Lebanon kufanyaje mara, n.k...Kazi unayo kwa kweli. Si uende tu huko Iran ukaishi kwa Ayatolah.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom