Iran kuwatia adabu wanaochochea vita

Iran kuwatia adabu wanaochochea vita

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Zarif: Iran itawatia adabu wachocheao vita

Muhammad Javad Zarif
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amemwambia Rais Donald Trump wa Marekani kwamba Iran haitaanzisha vita lakini itawatia adabu wanaochechea vita.

Muhammad Javad Zarif amejibu madai ya Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya Iran na kuandika katika ujumbe wake uliotolewa leo kupitia ukurasa wa Twitter kwamba: Bwana Trump! Angalia usije ukapotoshwa tena na wanaopenda vita daima, Iran inao marafiki, na hakuna mtu anayeweza kuwa na mamilioni ya "wapiganaji wa niaba".

Dakta Zarif ameongeza kuwa: Tofauti na Marekani inayosema uongo, kughushi na kupotosha, Iran inachukua hatua waziwazi na kwa msingi wa kujihami.

Jana Jumatano Rais wa Marekani alidai katika ujumbe wake wa Twitter bila ya kutoa ushahidi wowote kwamba: "Kwa mujibu wa ripoti na uchunguzi, Iran au askari wanaopigana kwa niaba yake wanapanga mipango ya kufanya shambulizi la ghafla dhidi ya askari au maeneo ya Marekani nchini Iraq, iwapo hilo litatokea, Iran italipa gharama kubwa."

Tags
DONALD TRUMP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maneno matupu hayavunji mfupa, wahenga walijisemea
 
Trump anatafuta ku-boost uwezekano wa kuchaguliwa mwezi Novemba. Labda tumwone atakachofanya.
 
Kuna jambo litafanyika hamtaamini mashia
 
Back
Top Bottom