Maneno hayabadilishi uhalisia.
Hapo zamani tuliambiwa, kamwe Israel haiwezi kuishambulia Iran, na kwamba ikithubutu kuishambulia, ndiyo utakuwa mwisho wa Israel. Kinyume chake, Israel ikaishambulia Iran, ikapiga kila ilipotaka. Aliyetajwa kuwa ni mbabe, Iran, ikaishia kurusha makombora hovyo, yakawaua waisrael 28, wote wakiwa raia, isipokuwa askari mmoja aliyekuwa likizo. Lakini mbabe huyo fake Iran, ikapoteza watu 1,190, na majeruhi 4,475 huku vifo karibia 600, vikiwa ni makamanda wa jeshi na wanasayansi wa nuclear.
Mwisho wa yote Iran akaamua kuwabembeleza wakuu wa Ulaya, waongee na Trump, ili vita ikome. Mbabe bandia Iran, akasema kutokana na vita hiyo, amesitisha ushirikiano na tume ya UN ya nuclear, lakini tishio dogo tu toka Israel kuwa kama Iran itarudi kurutubisha nuclear energy, kwa vile hakuna watazamaji, yenyewe itaitwanga tena Iran, mbabe fake amesalimu amri na kuahidi kutoa ushirikiano kwa tume ya UN ya nuclear.
Waarabu, kama maneno yao yangekuwa ndiyo vitendo, basi Israel isingekuwepo Duniani.