sandra B
Member
- Sep 29, 2014
- 80
- 68
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited imetoa msaada wa milioni 20 kwa ajiri ya kuchangia gharama za tuzo za wachezaji bora zinazotolewa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Akizungumza Dar es salaam jana katika makao Makuu ya IPTL kabla ya kukabidhi mfano wa hundi, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo Harbinder Sigh Seth alisema wameamua kutoa mchango huo kutokana na kuthamini dhamira ya TASWA kuwapatia tuzo wanamichezo kitu ambacho kinachangia kuongeza hamasa na kukaza michezo.
Alisema ingawa anajua gharama za kuandaa tuzo hizo ni kubwa, IPTL imeamua kutoa kiasi hicho kidogo ilikusaidia kutimiza azma hiyo na kuzitaka kampuni na wadau wengine kufanya hivyo ili kufanikisha tuzo hizo zinzotarajiwa kutolewa Desemba mwaka huu.
"Nimetoa mchango huu kwa kuwa mimi ni mpenzi wa michezo,nilikuwa nikishiriki mbio za magari na kuwa mshindi wa tatu katika mashindano ya Afrika", alisema
Jambo Leo