IPPMedia na Vichwa Vya Habari Mtandaoni

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Kwa wale tunaofahamu Historia ya vyombo vya habari Tanzania kwa hakika mtu hawezi kubisha kuwa IPPMedia ni moja kati ya vyombo vya habari vya mwanzo na vilivyokuwa makini Tanzania kwa kuanzisha tovuti. Kwa wale walio mbali na Tanzania ambao hupenda kufahamu kimejiri nini Tanzania, hakika watakubali kuwa Tovuti ni moja wapo ya njia nyepesi kabisa katika kupata habari za Tanzania kwa ujumla ukiacha SIMU na SMS kwa ndugu na jamaa waliopo Tanzania.

Hivi karibuni kumetokea tabia ambayo ama kwa makusudi au kwa kutokuwa na uwezo kwa IPP kuwanyima watanzania habari katika mtandao wao. Naam! Ninasema hivyo kwa sababu kuu moja, hii tovuti ni active na inakuwa updated kila siku na ina matangazo ya biashara mengi, Ila tovuti hii imekuwa ikichapisha vichwa vya habari tu, yaani ukitaka kufungua kusoma zaidi link au habari haipo. Inawezekana IPPMedia wanafanya hivi ili kuwafanya watu wanunue magazeti yao lakini wanatakiwa kujua kuwa uwezo wao wa kusambaza hayo magazeti ni Kwa Tanzania tu tena baadhi ya sehemu. Watu waliopo nje ya Tanzania hawawezi kuyapata hayo magazeti.

Ushauri:
1. Kwa nini wasiitoe tu hiyo Tovuti yao badala ya kuwaibia wafadhili wanaolipia matangazo yao kwenye Tovuti hiyo kwa kuchapisha vichwa vya habari na kuwafanya wasomaji wengi kutoingia kabisa kwenye Tovuti hiyo!

2. Kama ni mbinu ya biashara, kuwafanya watu wanunue magazeti yao basi wasambaze dunia nzima hayo magazeti na sisi tulio nje tupate kuyasoma, vinginevyo waweke habari katika mtandao wao kwani ni lengo la kufungua mtandao huo.

3. Kama wakiona haiwezekani basi wafiche kurasa zao kwa watembeleaji wa Tanzania kitu ambacho kinawezekana na watembeleaji wa nje wawe na access ya habari.

Nionavyo mimi kwa mtindo huu wa IPP kweli inaonesha kuwa sasa magazeti haya yanakoenda si kuzuri.
 
yes mkuu nami naungana nawe basi wafunge hiyo web yao.Mengi naona biashara sasa inamshinda kweli
 
Unchosema ni ukweli kabisa IPPMEDIA kwa muda mrefu wamekuwa magwiji wa kuwahabarisha si Watanzania tu bali dunia nzima. Lakini mtindo huu wa kuweka vichwa vya habari halafu habari yenyewe haipatikani haupendezi hata kidogo. Kama kweli wana masikio basi wasikie, kama nia ya kufanya hivyo ni kuwalazimisha watu kununua magazeti hiyo ni nia njema kwani wako katika biashara lakini kwa walio nje ya Tanzania kwa kufanya hivyo wanawanyima uondo wa kupata habari.

IPPMEDIA, funga hiyo website sisi tulioko Tanzania tusiione au tusome vichwa vya habari tu lakini wenzetu walio nje basi waweze kuifungua na kupata habari!!!! Kama hamjui ni jinsi gani hiyo inaweza kufanyika omba msaada.
 
yes mkuu nami naungana nawe basi wafunge hiyo web yao.Mengi naona biashara sasa inamshinda kweli

Utu uzima mkuu, mara nyingine hauna adabu unakupumbaza unakataa kukimbia huku unalazimisha wengine watembee kama wewe wakati haiwezekani
 
Kusoma habari kwenye website hatazuia mtu kununua gazeti hivyo IPP media waifungue hiyo tovuti pia itasaidia watu mbalimbali kutoa maoni yao kupitia tovuti hiyo.Kazi kwenu IPPmedia kuitikia maoni ya wadau wenu.
 
its true, ippmedia ilikuwa stable kuliko maelezo, but not anymore!! Mtuhabarishe basi kama mmeanza longo longo mbona hata globalpublishers huwa wanasema kama wamechemka kimtindo!
 
yes mkuu nami naungana nawe basi wafunge hiyo web yao.Mengi naona biashara sasa inamshinda kweli

IPPMEDIA walikuwa wa kwanza kuwa na tovuti ya magazeti yao mbali mbali, lakini sasa hivi wanaboronga ile mbaya. Unaona kichwa cha habari ukitaka kuifungua habari hiyo ili uisome haipatikani!!! Ni bora wafunge tu hiyo tovuti yao badala ya kuwa na tovuti ambayo haifanyi kazi kila siku iendayo kwa mungu.
 
Kama kuna ambaye ana link za magazeti ambapo tunaweza kupata habari za nyumbani naomba atuwekee.
 
Back
Top Bottom