Ipo wapi timu ya Cosmopolitans?

Ipo wapi timu ya Cosmopolitans?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,711
Reaction score
1,738
Wakuu, nakumbuka wakati naanza kupata ufahamu wa soka hapa nchi, timu iliyokuwa ikinivutia ni Cosmopolitans baadae ikapotea kimya kimya. Tafadhari mwenye kumbukumbu nzuri ya hii timu atupie hapa. Nilitonywa kuwa hata mhe Rage aliichezea timu hii kabla ya kwenda Msimbazi.
 
Mimi naulizia tuu Evaret ya Temeke Chang'ombe imeishia wapi. Hii ni timu ya mtaani ya wakina Juma Pinto,wakati yupo hapa Bongo na mambo yake hayajawa mazuri alikuwa wanapita huku na huko kutafuta misaada ya kuendesha timu. Lakini sasa hivi mambo yake yamekuwa mazuri Ughaibuni ndio timu imekufa kabisa hata kuikumbuka haikumbuki,kweli Wabongo wakishatusua hawaangalii walipotoka.
 
Kipindi hicho nilikuwa bado mdogo sana, nakumbuka timu kama Politan, Furaha, Cargo, Bandari, Temeke Squad, Likwati, Panama, Temeke Rangers, Shababi na nyinine nyingi, ilikuwa raha sana.
 
Mimi naulizia tuu Evaret ya Temeke Chang'ombe imeishia wapi. Hii ni timu ya mtaani ya wakina Juma Pinto,wakati yupo hapa Bongo na mambo yake hayajawa mazuri alikuwa wanapita huku na huko kutafuta misaada ya kuendesha timu. Lakini sasa hivi mambo yake yamekuwa mazuri Ughaibuni ndio timu imekufa kabisa hata kuikumbuka haikumbuki,kweli Wabongo wakishatusua hawaangalii walipotoka.

Tukiangalia upande mwingine wa sarafu, wabongo tupunguze kulaumu kwasababu fulani hatoi misaada. Kwa mtazamo wangu Evaret haiwezi kuendeshwa na misaada ya mtu mmoja eti mambo yake safi. Timu kama ile inatakiwa watu wenye moyo wa kujitolea , sio kwa mali tu kwa hali pia. Timu ya mpira imemshinda Kajumulo, wewe unatoa hela kwa ajili ya huduma ya timu watu wana njaa, maendeleo yatoke wapi?
 
Back
Top Bottom