Wadau nipo hapa Dodoma mjini baada ya kuondoka miaka takribani kumi iliyopita wakati nikisoma O level.Kipindi hicho kulikua na Radio Tanzania Kanda Ya Kati lakini nimeulizia hapa wenyeji wanasema haisikiki tena na hata frequency zake washazisahau.Nakumbuka kipindi hicho Radio Tanzania KandaYa Kati walikua washahama kutoka masafa ya AM kwenda masafa ya FM.Cha kufurahisha kwa sasa nimekuta utitiri wa Radio Stations Dodoma nadhani kwa sasa Mji wa Dodoma utakuwa unashika nafasi ya tatu baada ya Dsm na Mbeya kwa uwingi wa Radio Stations. Kuna Mwangaza Fm,Radio Uzima,Radio Maisha Fm,A-fm,Abm Radio,Dodoma fm,Ras Fm,Impact fm,Nyemo fm,Kifimbo fm n.kJe nini kilitokea hadi kufungwa kwa radio station hii ambayo ilikua inafanya vizuri tu enzi hizo ikiwa na watangazaji maarufu Leonard Leo,Marehemu Ben Kiko na wengineo...!!
Nawasilisha
Nawasilisha