Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,055
Najua mnajua kuhusu suala la mafaili anayolala nayo kitandani. Maana ameshalirudia si chini ya mara moja.
Kwa tafsiri nyepesi kabisa, anachojaribu kuonesha ni kwamba yeye ni mfuatiliaji na sio mtu wa kuamini taarifa za kupewa kwa muhtasari. Anazama mwenyewe.
Tusijeshangaa siku moja, aidha kwa uchovu kwa kutaka tujue uzito wa maneno yake, ataalika waandishi wa habari Ikulu na kuwapeleka mpaka chumbani anapolala kisha aoneshe hayo mafaili.
Ni dhahiri, hicho ni kilio cha kuomba msaada (a cry for help) kutoka kwa kiongozi wetu. Je, anataka tumsaidiaje?
Nadharia nilizonazo;
1. Muda: Mafaili ni mengi maana yake mambo ni mengi ya kufanyia kazi hivyo yanahitaji muda mwingi ili yote yaweze kutekelezwa. So, tumuongeze muda wa kuyafanyia kazi. Miaka 10 inaweza isitoshe.
2. Uaminifu: Ofisi yake haimpi imani ya kutosha kuweza kusaidiana nae kuchakata masuala nyeti ya kitaifa, hivyo anahitaji kueleweka pale anapoamua kufanya maamuzi ya kuwabadilisha badilisha. Zipo tetesi pia kuna watumishi wanatoka kumfanyia figisu.
3. Pride: Huenda kwake ni fahari kuwaambia watz ni namna gani anafanya kazi usiku na mchana kiasi cha kujaza vitendea kazi mpk sehemu anayolala. Lengo ni kupata kukubalika!
Tumsaidieje?