iPhone za Makumbusho zina nini?

Iko hivi mkuu iphone nyingi za maeneo ya makumbusho pale ni refurbished (used then zikarejeshwa kiwandani kwa ajili ya marekebisho) hapa wanabadili betry na kava so simu itaonekana ni mpya kabisa na wanazitoa kutoka china hizi refurbished,
Refurbished iphone ina faida ina hasara zake pia ila kama unataka iphone ambayo siyo refurb basi lazima uchane mfuko kweli kweli mkuu ndiyo utapata kitu chenyewe kilichokuwa kimesimama.
Kila la kheri mkuu
 
Kinachofanyika hapo kwa hizo refurbished ni wanakutafutia box la iphone na mara nyingi linakuwa box jeupe tu lenye neno iphone kwa pembeni na vifaa vya sim kama chaja na earphone.
Faida ya refurbished iphone ni kupata kumiliki iphone kwa bei rahisi saana,
Hasara zake kama betry iliyobadilishwa siyo original basi baadaya mda betry huvimba na kuharibu kioo cha simu.
Usiogope mkuu pia kama una kismati unaweza kupata refurbished na ikadumu fresh kabisa kwa mda mrefu ila ni bahati saana kuipata ya namna hii.
 
Habari zenu wanazengo, naombeni kupata ufafanuzi kidogo kuhusu iPhone zinazouzwa madukani makumbusho dar...nilikuwa nataka kununua ila nikafanya utafiti kidogo wengi wakaniambia nenda makumbusho

Ila kabla sijaenda nikatonywa na fundi wang wa simu akasema usiende kule watakupa simu feki, mara wengine wanasema second hand, mara refurbished, mara hazidumu kwa sababu sio orijino.
naombeni mnisaidie jaman nijue kiundani zaidi kama kuna aliyewah kununua na kujua mapunguf ya hzo simu..na pia mnielekeze sehem wanazouza hizi simu original kwa bei ya kawaida maana ni ndoto yangu na mimi kumiliki iphon... iphone 5,5s au 6 zenye storage ya 16 had 64
sijaandika huu uzi kwa lengo la kuharibu biashar ya wtu
nsamehen kw mwandiko wang kama utawakera
WEWE NAE UNAUDHI...KWANI UMEAMBIWA MAKUMBUSHO TUU NDIO WANAUZA SIMU ZA iPHONE? Maduka mengine huyaoni?
 
Hivi kuna nini cha ziada iphone kuizidi sana Sansung? Nimeuliza kizushi, kwa sababu nilinunua iphone 6 sikudumu nayo nikaiuza.

Tunaoshinda jf wala haifai. Kushinda unabofyabofya haipendi, beteri lake goigoi, halafu ukizima ukaweka chaji, inajiwasha automatic, sasa ndiyo nini!
Lakini ukikuta wenye alosto nazo kusifia!

Uzalendo ulinishinda nikaita dalali.
Tangia hapo nikang'ang'ania samsung mazima kwa sababu wananipatia ninachokitaka.
 
Kifupi hizo simu sio feki ila zimekuwa refurbished me nilichukua hapo I phone 6 mpaka leo ni mwaka wa pili sijapata tatizo lolote jamaa anakupa na warant wala hamna shida
 
kusema ukweli mimi nilienda kununua samsung pale mwezi wa pili, ila Ndo hivyo tena, naweza kusema nilipigwa! Simu inayouzwa Tsh laki 4 hadi laki 3 niliuziwa kwa laki sita! kipindi hicho nilikuwa sijajua bei vizuri, Halafu simu yenyewe nilouziwa ni china Version, yaani imejaa uchina ni hatari, Mwanzo sikuwa hata na uwezo wa kuupdate ila baada ya kuipiga spana sana sasa iko sawa kibishi
 
Nenda Kariakoo China Plaza, kuna maduka mengi ya IPhone original kama Punga phone na mengine mengi tu, utapata IPhone X, IPhone XS, IPhone XSM na matoleo mengine ya kisasa ZAIDI, achana na used au fake utapoteza pesa yako bure
 
Habari zenu wanazengo, naombeni kupata ufafanuzi kidogo kuhusu iPhone zinazouzwa madukani makumbusho dar...nilikuwa nataka kununua ila nikafanya utafiti kidogo wengi wakaniambia nenda makumbusho

Ila kabla sijaenda nikatonywa na fundi wang wa simu akasema usiende kule watakupa simu feki, mara wengine wanasema second hand, mara refurbished, mara hazidumu kwa sababu sio orijino.

naombeni mnisaidie jaman nijue kiundani zaidi kama kuna aliyewah kununua na kujua mapunguf ya hzo simu..na pia mnielekeze sehem wanazouza hizi simu original kwa bei ya kawaida maana ni ndoto yangu na mimi kumiliki iphon... iphone 5,5s au 6 zenye storage ya 16 had 64

sijaandika huu uzi kwa lengo la kuharibu biashar ya watu,

nisamehe kwa mwandiko wang kama utawakera
Kwanza kabisa usinunue iphone 5 wala 5c maana apple ashaacha kuzipa support pia iphone5s ina support ila nayo huenda ataacha hivi karibuni maana apple anatabia ya kusupport simu kwa miaka 5 toka ameitoa. Hivyo chini ya iohone 5s hazipokea updates na apps nyingi kwa iohone 5 kurudi nyuma hazisupport.
Nunua kuanzia iphone 6, kuhusu fake iphone ni ngumu kuuziwa iphone fake maana kama umeshawahi kutumia iphone ni rahisi sana sana kujua kuwa hii ni fake kwakuwa watafake umbo lakini ios wataishia kuweka tu theme kitu ambacho ni rahisi kugundua.
Ila inawezekana labda wanawauzia simu refurbished au zilizorekebishwa na hilo litakuwa kweli maana haiwezekani simu mpya iuzwe labda milion moja laki nane wao wqkuuzie laki tisa na nusu.
 
Mkuu simu refurbrished sio feki.
Ujue iphone washaacha kuzitoa izo iphone 6 7 8 etc so unazoziona kwenye market nyingi huku mjini ni refurbrished tu ni ngumu sana kuikuta iphone 6 ambayo sio refurbrished kws kuwa iphone walishaacha kuitoa kitamboo.
Nenda wstakupa warranty ya mwaka au miaka miwili ikisumbua utapewa mpya
Kama una force mnoo unataka ambayo sio refurbrished nakushauri sehemu pekee ni apple store mlimani city ambako bei yake hutoiweza kwa sababu nakuskia ukilalamika lalamika bei. Sasa kule wanauza iphone 6 mpaka laki 7 na nusu wakati simu hiohio makumbusho ni laki 4 utaweza????
Ushauri wa bure nenda mlimani city kama huna pesa nenda makumbusho uache kusumbua watu
 
Back
Top Bottom