Ipende na ilinde simu yako

GMBDC

Member
Aug 13, 2012
14
0
Ndugu Watanzani
Karibuni kwenye huduma yetu mpya ya kuhifadhi udhamini (warranty) za simu. Wadau wengi wamekuwa wakinunua simu na kupewa udhamini wa muda fulani wa simu zao. Ila pindi wakipoteza stakabadhi ama kadi za udhamini (warrant card), Inakua ngumu kufanya marejeo ya muda wa ukomo wa udhamini. Hivyo tatizo hilo tunalimaliza kwa kuweka mfumo ambao kila mtanzania anaweza kuweka kumbukumbu zake za udhamini(warranty). Kwa kuanzia tunaanza na simu na baadae vifaa vingevyo kama laptop, TV, Fridge, n.k vitawekwa.

Faida zake ni nyingi ila chache ni kama zifuatazo

  1. Unaweza kupata kumbukumbu ya udhamini wako bila kusumbuka
  2. Vile vile ukipoteza simu yako (blackberry, IPAD, Nokia, Samsung Gallaxy, n.k) unaweza kuipata IMEI yako kiurahisi sana na kwenda kwa watu husika kwa ajili ya kublock simu hiyo isitumike
  3. Vile vile simu yako ikipotea aliyeiokota anaweza kukupata kwa kutumia IMEI number kupata simu number yako.
  4. Vile vile kwa wale wanaouziwa simu(vimeo) either zimetumika zikavishwa kava mpya ukaambiwa ni mpya ama mtu kaiba simu then anataka kukuuzia bado unaweza kufahamu aliyekua anaitumia kabla (kama alisajili kwenye mtandao wetu)
  5. Unaweza kupata historia ya wamiliki wa simu kama imemilikishwa kwa mtu zaidi ya mmoja na wote walijisajili


JINSI YA KUFANYA
KWA SIMU MPYA
Nenda sehemu ya kuandika ujumbe mfupi kisha andika kama ifuatavyo
reg*Aina ya simu*modeli ya simu*IMEI number YAAANI Reg*Nokia*Tochi*254367746364759
Kisha tuma kwenda 15568 kisha utapata ujumbe wa ukikuambia sasa umesajiliwa.

KUJUA UDHAMINI/WARRANTY
Tuna neno: Warranty*IMEI NUMBER YAANI warranty*276485985765990
Kisha tuma kwenda 15568 utapata ujumbe ukikwambia warrant yako inaanza lini na inaishia lini

KWA WASIO NA SIMU MPYA
Kwa wale ambao simu zao tayari muda wao wa udhamini umeisha ama wamenunua siku nyingi. Unachotakiwa kufanya ni kusaijili tu simu yako ili kuendelea kupata faida nilizozitaja hapo juu.

Tuma Neno: Sajili*Aina ya simu*modeli ya simu*IMEI number yaani Reg*Nokia*Tochi*254367746364759
Kisha tuma kwenda 15568 na utapata ujumbe wa kukuhikikishia kwamba umesajiliwa.

Angalizo:

  • utaratibu huu umeanza kutumika baadhi ya maduka ya simu nchini.
  • Jinsi ya kufahamu IMEI yako andika *#06# utaipata (IMEI=SERIAL NUMBER)
  • * ni alama ya nyota
  • Hakuna gharama nje ya ujumbe wa kujisaji ama kuulizia warrant au IMEI yako
  • Hakuna Garama za kila mwezi wala hakuna gharama zozote za kificho.
  • Huduma hii inatozwa TZS 250/= kwa kila ujumbe utakaotuma na makosa yatatozwa.
  • Huduma hii ni Kwa watumiaji wa TIGO na VODACOM kwa sasa (Zantel na Airtel kufuata baadae).
 
Kwa faida ya wote,
waliotutumia pamoja na kujibu email zenu tunapenda kutoa baadahi ya ufafanuzi hapa.

  1. Swali kuhusu Warranty. Tunachofanya ni kuhifadhi kumbukumbu ya lini warrant yko inaanza na lini inaisha na jinsi ya kufanya kudhibitish hilo andika reg(nyota)aina ya simu(nyota)modeli ya simu(nyota)IMEI namba kisha tuma 15568
 
Kuhusu nafasi kati ya neno moja na jingini

Mfumo wetu unatenganishwa na nyota bila kuacha nafasi yaaani reg*blackbery*9700*123456789876543 kisha unatuma kwenda 15568
 
kuhusu reply

Unapotuma ujumbe reg*Nokia*N95*74747474748583 ama sajili*nokia*Ringo*26354785889987556 kwenda kwenye number 15568 utapata ujumbe kukutaarifu ombi lako limepokelewa.
 
Kuhusu aina ya simu

Mfumo wetu ni kwa ajili ya simu zote yaani Nokia, Sumsum, Techno, Blackbery, HTC etc hakikisha tu wakati unaandika
ujumbe useme aina ya simu unliyonayo. Kama ni Nokia Music express, Blackbery Bold, HTC chacha n.k na ujumbe utakaopata utakujulisha aina ya simu uliyoregister
 
Kuhusu Zawadi,

Ni kweli tutakua na zawadi tatu kila mwezi ambazo zinaweza kuwa ni simu ama fedha taslimu kama itakavyoamuliwa. ikumbukwe pia zawadi kama ni simu itakua brand uliyosajili, yaani kama umesajili Blackbery basi zawadi ya simu itakuwa ni blackbery ambayo thamani yake ni kubwa kuliko uliyoisajili lakini isiyozidi millioni moja.
 
Swali la mwisho: Unaweza kijisajili mara ngapi

Kama tulivyosema tangu awali lengo la kujisajili ni kuilinda simu yako uweze kupata warrant stahiki
ama mwenye simu aweze kupatikana kirahisi pale simu inpopotea na faida nyinginezo. hivyo kujisajili ni mara moja tu
isipokua unamuuzia simu yako mtu mwingine anaweza kuisajili tena. Kuuliza usajili ama ukomo wa waranti(udhamini) wako unaweza kufanya mara nyingi uwezavyo.
 
Wakuu sijui kama haijaeleweka naona maswali ya namna ya kujisajili yankua mengi ni

reg*aina ya simu yako*modeli yake*imei number hakuna kuacha nafasi. tumia mfano
huu.

reg*samsung*galaxy*350252563365348

Note: imei ni digit 15 na unaweza iona kwa kupiga *#06#

naomba refer post number 1 &5 hapo juu
 
Aiseee Wakuu, hii kitu ya hawa jamaa inafanya kazi, Nilidhani ni uchakachuaji lakini leo kuna Bint ofsini kwetu
alisahau(aliibiwa) BB yake kwenye dala dala, sasa katika harakati za kuiza kariakoo conicidence kuna mkaka alitaka
kuinunua ndio akarequest number ya user kwa hawa jamaa. Ikampatiawalivyompigia kucomfirm kama yeye ndiye alietaka kuuza simu, jamaa wakaingia mitini. Mkaka kaipeleka ile simu police Msimbazi mwenye ndio kaichukua simu sasa ivi. Thank you guys, Mungu awabaribi mnooooooooooo na mungu aibariki JF maana bila JF hata hizi habari tusinezijua
 
Unapokuwa na details hizo zote maana yake unaweza kumtrace mmiliki wa simu hiyo!!!!!! Uongo? Ngoja nitarudi nahofia pasije pakawa na kitu nyuma ya pazia!!!!!!
 
Naona unajiuliza na kujijibu mwenyewe maswali!!!....bado haujasomeka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom