Msuya: Uongozi na serikali yenu vinanuka si puani tu bali hata masikioni.
Pinda: Mheshimiwa mzee, sijakuelewa. Ni fumbo umenipa. Naomba nisaidie.
Msuya: Serikali yenu mlivyo ni kama mtu mzima mzima aliyetoa ushuzi kati ya wenzake mliokaa katika maongezi. Akiingia mgeni mara, kwa atasikia harufu ya mnuko kisha akiwaangalia usoni kila mtu ameukunja uso. Ni mwenye ujasiri, mmoja ama wawili, tu ndiye anayeweza kuendelea na mazungumzo.
Wapo walio**mba, nyote mnanuka. Suluhisho si kunyamaza kimya bali ni kumtafuta na kumfukuza kama hataki kujiondoa kwenye kijilinge chenu.