iPad Users

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2011
Posts
3,216
Reaction score
994
Need a help!

I have a new iPad activated in US, it has a cellular mode but the chip is from apple. Can I have a local cellular chip cut in that shape from any provider (eg Airtel, Voda). Nisaidieni nimeambiwa kuna kifaa wataalamu wanatumia kukata simcard za airtel au Vodacom ili iweze kuwekwa katika hii iPad, kwasasa natumia wi-fi lakini sehemu nyingi hapa kwetu hatuna wi-fi.

Wasalaam,

Nashukuru nimepata microchip ya vodacom na inachapa kazi. Kuweka bundle ni rahisi tu, unatumia lini nyingine unainunulia bundle unayotaka kama ni siku,wiki au mwezi. Tumia mpesa ni rahisi tu. Kwangu mimi hii ni 100 maana nataka kwajili ya internet tu japo pia kwa kutumia viber naweza kupiga simu
 

Uko wapi kwa sasa? Mimi nipo hapa Morogoro, kuna jamaa anakata hizo line!
 
Tembelea office za Voda au Airtel utapata line bila matatizo sio lazima ukate.
 
Kama upo Dsm nenda airtel, MLIMANI au popote penye ofisi zao wanazo SIM card "micro" kwa ajili

ya iPad.
 

Kama wataka micro simcard zipo tayari na huna haja ya kukata,ila kama ni shida yako kukata nenda airtel moroco pale nshakatiwa bureeee,cha msingi nenda ofisi za wateja za mtandao unaotaka kutumia baaasi utanunua hiyo micro simcard au utakatiwa mini simcard yako bureee.
 
Pia ningependa kujua kama nahitaji software maalum ambayo nitakuwa natumia ku access hiyo simcard nitakapokuwa nahitaji kuweka pesa hasa bundle.
 
Asante Bob Kinguti, niko DSM ila nadhani nitakuja Moro wiki hii nielekeze yuko wapi.

Ukifika Moro, nenda Piras Supermarket. Ukiwa maeneo hayo uliza duka la samsung items. Opposite na duka hilo ndio jamaa aliko. Anaitwa Adili.
 
Kata mwenyewe kaka, tunaishi kwenye ulimwengu wa DIY (Do It Yourself), unachotakiwa ni kuwana na template ambayo unaweza kuitengeza kwa kutumia kadi yako ya Marekani, kisha uwe na msumeno mdogo au kisu ukiweke kwenye moto na tupa, unakata kufuata template kisha unaichonga na kiweka sawa kwa tupa, moto mbele.

Mimi nilifanya hivyo miaka ya nyuma, hivi sasa kwenye Ebay au Amazon kuna aina fulani ya kifaa (kinaonekana kama stepler) ambacho kinauzwa hivyo kabla ya kuondoka Marekani ungenunua kifaa hicho kazi ingekuwa rahisi maana unatumbukiza kadi ndani ya kawaida na kuibana inakwatwa na kijistepler hicho ambacho kinaitwa Sim Cutter.

Good Luck
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…