Safi sana chief. Unajua hivi vitu watu wengi hawavifahamu, mtu anajua ukishalipia tangazo tu facebook basi ni lazima upate sales. Hii ni knowledge ambayo watu wanatakiwa kuipata ili waweze kufanikiwa kwenye kufanya marketing kupitia hiyo mitandao.
Kuna kitu umekieleza hapo mwanzo kuhusu purpose au intent ya tangazo, Watu wengi huwa wanakimbilia kuwa na Sales intent bila kujua who actually wants to buy their products, yaan unakuta mtu anataka kufanya sales lakini hajui ni nani hasa anahitaji bidhaa anayouza, hii inapelekea lile tangazo kuonekana na watu ambao hawana interest na bidhaa au huduma anayoitoa, kwahiyo watu wanaishia kulike tu bila hata kuclick link ya tangazo. Kwahiyo ni muhimu kwanza kujua interest na demographics za wateja unaowalenga.
Namshauri mtu ambaye ana purpose ya kufanya sales aanze na Engagement Goal ili kupima maji kwanza kabla hajaamua kuja na sales goal.
By the way hongera, unaonekana unafahamu vitu vingi sana, niko tayari kujifunza kutoka kwako, tupe maarifa watanzania wenzako, mungu atakubariki.