Interview ya Paul Makonda na E-FM Radio

Interview ya Paul Makonda na E-FM Radio

chagga land

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2015
Posts
394
Reaction score
95
Wadau,

Muda si mrefu mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda atakuwa live E-FM radio akizungumzia maswala mbali mbali. Tujumuike pamoja katika uzi huu nitawaletea atakachozungumza.

========

Ameshaanzaa kuongea muda huu, na anasema mabadiliko yaliyopo sasa hayaepukiki kabisa na wapo watakaoumimia na kufikia majanga tofauti tofauti.

Anasema amekuja na kampeni maalum ya safari checkup ambayo itajihusisha na urekibishaji wa magari ili kuzuia ajari kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Amesema kuwa nia ni kurekebisha afya ya magari yetu.

Amesema kuwa safari checkup itafanyika maeneo ya Coco ambapo mafundi karibu wote wa magari wa Kinondoni watakuwepo hapo.

Mh. Makonda ameungana na mmoja wa mafundi wa magari nae amesema wamelipokea wazo la mh na amekubali na kuwashirika wamiliki na mafundi zaidi ya 15 ambao watashiriki zoezi hilo hapo Coco.

Fundi huyo pia amesema safari checkup itafanyika bure kabisa kwa siku ya kesho na keshokutwa.

Mtangazaji, Gardner G. Habash, anampogeza mh Makonda kwa kuja na wazo zuri sana katika msimu huu wa sikukuu ambao hutawaliwa na ajali sana kutokana na ubovu wa magari yetu.

Pia mh. Makonda amesema kuna watu katika hii nchi wanaishi kwa matukio na wengine wanaishi kwa malengo. Amesema kumsingizia mtu kwa kutumia resource zako si vizuri, kama jana kuna gazeti amesema aliliona likiwa na picha ya mtu mwingine na picha inasema kuwa ni yeye alipokuwa akiutafuta ukuu wa wilaya.

Ameongeza kuwa yeye anawatumikia wananchi na jana amesema amevumbua ufisadi wa mabilioni ya fedha. Pia ameahidi kuwa yeye hana jazba, hajikuzi ila yupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Makonda amesema yeye ni mdogo kuliko kazi anayofanya. Anasema tuwaache watu wanaoenda na matukio lakini anawahusia wanakinondonW kujikita katika maendeleo na kuachana na wanaoendana na matukio.
 
Sumatra imepata msaidizi. Vp juu ya 'sembe'?? Uchangudoa??
 
Back
Top Bottom