Uncle Rukus
JF-Expert Member
- Jun 16, 2010
- 2,415
- 398
Mimi ni mtumiaji mzuri wa huduma za tigo hasa huduma ya internet , nimekuwa mtumiaji wa package ya standard month tsh 40,000/- (kabla hawajabadilsha bei )kwa takribani miezi 8 hivi hadi walipo badilisha mashart na kutoa 4gb only, nikahamia max month kutokana na matumizi yangu kuwa juu nikaona hii ndio package inayonifaa kwa matumizi yangu.
Nimetumia package hii ya max month tsh 100,000 (15 gb )kwa miezi 4 hivi, toka wiki iliyopita speed yake imekuwa ndogo sana na uwezi kufanya chochote cha maana na hata kwa siku ukiacha computer on uku ukidownload uwezi maliza kudownload file la 700mb , ukiangalia gharama ya hii package na huduma tunayopewa haviendani kabisa huu ni wizi kabisa sijui TCRA wanafanya kitu gani wakati wananchi tunaibiwa mchana kweupe na haya majambazi ya huduma za mitandao.
Ukiwasiliana na huduma kwa wateja kitengo cha data hawana majibu ya kueleweka na hawana msaada wowote zaidi ya kukuambia "chomoa modem na uchomeke tena"
Je kuna wadau wengine mmekutana ka na tatizo ili ya kushuka kwa speed ya mtandao wa tigo?