Uko wapi na unahitaji ya komputa ngapi ? hizi nyingi hawauzi madukani lakini unaweza kununua kwenye mtandao kuna hata programu huria nzuri sana kwa ajili ya kufanya kazi hiyo .
Ukisema za free zinasumbua elewa kwamba hata za kununua zinasumbua. chukulia mfano mdogo wa OS windows na Ubuntu. Je ukitumia windows ambayo si ya bure unakuwa guraanteed kuwa haitasumbua? Jibu ni No......
Na hizo ulizzotumia zilizo kusumbua ni program gani. zitaje wadau wenye uzoefu wa biashara ya internet watakupa majina ya program "nzuri" nyingine
vile vile Kabla ya kuuliza wapi unaweza kununua kwanza ulizia jina la software hiyo "nzuri" . then Isome review zake kwenye mtandao ujirizishe then kaiununue. Maaana Ukishanunua ndo imetoka.
Mkuu ukisema za free zinasumbua unakosea, nimetumia timewatcher ya free more than 10 yrs na haijawahi kuniletea shida, wewe unatumia Time watcher gani?
Zipo za kudownload ambazo ni nzuri pia zinakuwa na serial zake lakini ambazo ni za free kuwa wajanja wanajua namna ya kuzifungua kitu ambacho kinaweza kikawa kinakuletea hasara mkuu!
Zipo za kudownload ambazo ni nzuri pia zinakuwa na serial zake lakini ambazo ni za free kuwa wajanja wanajua namna ya kuzifungua kitu ambacho kinaweza kikawa kinakuletea hasara mkuu!
Mkuu kwa sasa Natumia Time watcher kwa jina ni Time Watcher(Cyber cafe Software)-Business Version 5.1 ambayo nimei download kupitia http://www.timewatcher.de/bus/Home/ ina option ya Administrator and Client Version wakati wa kuinstall..tatizo nalopata ni kustack mara kwa mara..na kuleta error messages nyingi..labda mkuu uliyetumia kwa miaka kumi unieleza unatumia Time Watcher ya aina gani..na kwa computer ngapi?