Intelligence unit Tz iko wapi?

BASHADA

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
513
147
Imekuwa kawaida sasa kusikia serikali ikikataza maandamano ya vyama vya siasa kwa kile walichoita "sababu za kinteligensia' kuwa wangevuruga amani na mambo mengine kama hayo. Mshangao wangu ni kuwa meli ya Spice Islanders ilipopakia abiria wengi vile zaidi ya 3000 (kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi) serikali haikuwa na inteligensia? Au intelligensia imehamia kwa chadema tuu. kwingine kote kumepigwa off.

Magari mabovu hakuna inteligensia, meli mbovu hakuna inteeligensia, madawa ya kulevya hakuna intelligensia, machangudoa kwenye madanguro hakuna intelligensia, pesa zinakwapuliwa BOT hakuna intelligensia, wanafunzi wanafeli hakuna intelligensia, jamani, hebu na mengine jazeni, kote hakuna intelligensia?
 

mmbangifingi

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
2,839
554
Hayo mengine hayana maslahi kwa watawala, "kama ni wanafunzi kufeli acha wafeli tu" thats why inakosekana intelijensia. Huoni wanavofurahia na kuwafanya mtaji wananchi wajinga inaokuwa rahisi kwao kuwadanganya nyakati za chaguzi kwa ubwabwa,kofia,vilemba na ti shirt?
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom