Intaneti ni tishio kwa Watawala au tatizo la uelewa wa Demokrasia?

Intaneti ni tishio kwa Watawala au tatizo la uelewa wa Demokrasia?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
Katika miaka ya karibuni, kuzimwa kwa intaneti wakati wa uchaguzi kumegeuka kuwa jambo la kawaida katika baadhi ya nchi za Afrika. Mataifa kama Tanzania na Uganda yameshuhudia kufungwa kwa mitandao ya kijamii au kuzimwa kabisa kwa huduma za intaneti kipindi ambacho wananchi wanahitaji taarifa zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hali hii imeibua mjadala mpana kuhusu hatma ya demokrasia na haki za msingi za wananchi.

Mifano ipo wazi. Uganda ilizima intaneti na mitandao ya kijamii wakati wa uchaguzi wa mwaka 2021 na imefanya hivyo 2026, ikidai sababu za kiusalama. Tanzania, katika chaguzi zilizopita, ilishuhudia upatikanaji mdogo au kufungwa kwa majukwaa kama X (Twitter) na WhatsApp JamiiForums, uchaguzi Mkuu 2025 internet ilizimwa kabisa, hali iliyodhibiti kwa kiasi kikubwa mawasiliano ya wananchi.

Ethiopia pia imekuwa ikizima intaneti mara kwa mara, si tu wakati wa uchaguzi bali pia wakati wa migogoro ya kisiasa, hali iliyonyima mamilioni ya watu taarifa muhimu.Nchi nyingine kama Sudan, Guinea, Chad na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimewahi kutumia mbinu kama hiyo.

Kinachofanana katika mifano hii ni hofu ya taarifa huru na uwezo wa wananchi kufuatilia na kuripoti mwenendo wa uchaguzi kwa wakati halisi. Badala ya kuzima uvumi, hatua hizi mara nyingi huongeza sintofahamu na kuimarisha hisia za kutokuaminiana kati ya serikali na wananchi.

Kuzima intaneti kunakiuka haki ya msingi ya kupata na kusambaza taarifa. Katika zama za kidijitali, intaneti si anasa bali ni miundombinu muhimu ya kiraia, sawa na barabara au umeme. Kuizima ni sawa na kuzima sauti za wananchi wakati zinapohitajika zaidi.

Intaneti si tishio kwa demokrasia, bali ni kioo kinachoonesha uhalisia wa uongozi. Changamoto kubwa ni uelewa duni wa thamani ya uwazi na uwajibikaji. Badala ya kuzima intaneti, serikali zinapaswa kujenga mifumo imara ya uchaguzi inayokubali uhakiki na ukosoaji wa wazi kama nguzo ya demokrasia ya kweli.
 
Hoja iko hapa👇🏻, (nanakuu paragraph ya mwisho ya andiko lako)

"...Badala ya kuzima intaneti, serikali zinapaswa kujenga mifumo imara ya uchaguzi inayokubali uhakiki na ukosoaji wa wazi kama nguzo ya demokrasia ya kweli.."

Na hii maana yake ni kuwa:

√ Serikali zenye tabia hii, zinajua fika kuwa chaguzi hizi huwa ziko manipulated kwa zaidi ya 90%. Na kwa sbb hiyo siku za uchaguzi hudhibiti flow ya taarifa ili watu wapokee taarifa za wale tu waliondaliwa na watawala kutupa taarifa za uongo, zisizo na ukweli..

√ Ni bahati mbaya kuwa, kwa Tanzania Oktoba 2025, hawakufanikiwa kulifanya hili kwa ufanisi, waliumbuka na uongo wao wote uko hadharani kuanzia takwimu za uchaguzi kutokuakisi hata chembe ya ukweli na pia kile kilichofanyika gizani wakiwa wamezima internet, kutokana na maendeleo ya teknolojia ya habari, baada ya mfumo wa mawasiliano kurudi, kila kitu kiliwekwa wazi!
 
Mifano hai ya utawala za kidikteta zinapoamua mambo bila kujali athari zake

Uhaba wa bidhaa wanukia Uganda agizo la kuzima intaneti likikwamisha mizigo Kenya​

Na gazeti la TaifaLeo
mizigo-uganda.jpg

Shehena za mizigo katika Bandari ya Mombasa. Hatua ya Uganda kuzima intaneti imeathiri usafirishaji mizigo. Picha|Maktaba

WAHUDUMU wa mizigo katika Bandari ya Mombasa wamesitisha usafirishaji wa mizigo inayoelekea Uganda na nchi nyingine zisizo na bandari, saa chache baada ya taifa hilo kuzima huduma ya intaneti kabla ya Uchaguzi Mkuu wa leo.

Mawakala wa kuthibitisha na kuondoa mizigo bandarini pamoja na wasafirishaji walisema hatua ya mamlaka za Uganda kuzima intaneti kitaifa ilikatiza mawasiliano kati yao na madereva, na kuvuruga taratibu za kuunda nyaraka na uidhinishaji wa mizigo.

Mwenyekiti wa kitaifa wa Chama cha Kimataifa cha Usafirishaji Mizigo na Uhifadhi wa Maghala nchini (KIFWA), Bw Fredrick Aloo, alisema sekta hiyo hutegemea sana intaneti na mizigo haiwezi kusonga bila mawasiliano.

“Intaneti inapozimwa, uratibu unakuwa mgumu zaidi, ufuatiliaji na uwasilishaji wa nyaraka unachelewa, na safari huchelewa,” alisema Bw Aloo.

Mbali na mawasiliano, Bw Aloo alisema mizigo ya kusafirishwa kwenda nchi jirani hutegemea vifaa vya ufuatiliaji vya GPRS vinavyotuma taarifa kupitia data ya simu na intaneti.

“Bila intaneti kuna hatari ya msongamano mkubwa katika vituo vya mipakani,” akasema.

Mnamo Jumanne, serikali ya Uganda iliagiza kampuni za mitandao ya simu kufunga huduma ya intaneti ya umma kuanzia saa kumi na mbili jioni huku shirika la kufuatilia matumizi ya intaneti, NetBlocks, baadaye likithibitisha kuwepo kwa “usumbufu wa kitaifa wa huduma ya intaneti”.

Bw Roy Mwanthi, msafirishaji wa mizigo kutoka Mombasa, alisema kwa sasa anaelekeza juhudi zake katika kusafirisha mizigo ya ndani ya nchi hadi baada ya uchaguzi.

“Mizigo ambayo tayari imeidhinishwa kwa safari ya nje ya nchi itasafirishwa hadi mipaka ya Busia na Malaba, lakini ili kuhakikisha usalama na kuepuka hasara, tutaelekeza nguvu zetu kwenye mizigo ya ndani,” alisema.

Uchaguzi huo wa urais unaonekana kama marudio ya kinyang’anyiro cha mwaka wa 2021, ambapo Rais Yoweri Museveni, 81, ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne, anakabiliwa tena na mpinzani wake mkuu, mwanamuziki Bobi Wine, 43, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi. Kuna wagombeaji wengine sita.

Mamlaka ya mawasiliano ilitetea uamuzi wake kwa msingi wa usalama wa umma ili kuzuia “upotoshaji wa taarifa mtandaoni, habari za uongo na udanganyifu wa uchaguzi, pamoja na kuzuia uchochezi wa vurugu”.

Mapema mwezi huu, mamlaka hiyo ilipuuza habari zilizokuwa zikienea kuhusu uwezekano wa kuzimwa intaneti wakati wa uchaguzi ikidai kuwa ni uvumi, na kusema jukumu lake ni kuhakikisha mawasiliano yanapatikana bila kukatizwa kote nchini.

Katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2021, ambao ulighubikwa na maandamano makubwa yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa, huduma ya intaneti ilikatizwa kwa angalau wiki moja.

Hali sawa na hii ilishuhudiwa mwaka uliopita wakati vurugu zilipotokea baada ya Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania, ambapo pia wasafirishaji mizigo kati ya Kenya na nchi hiyo jirani walitatizika katika mipaka kama vile Lunga Lunga na Taveta.
TaifaLeo
 
Back
Top Bottom