Tatizo ni kwamba watanzania walio wengi hatujui maana ya bima na ndio maana makampuni ya bima hapa nchini yanafaidika sana kwa hilo.
Hii ni kweli. Hata kwa wachache wanaojua maana ya bima na kuzinunua, wengi wao hawajali kusoma ile mikataba. Kwa hiyo anapopata janga ndo anaanza kuhangaika, ninachojua kila janga lina
sera/mkataba wake na
taratibu zake za kudai bima endapo limetokea hilo janga husika.
Kuna uzembe na kuzungushwa ktk kudai bima lakini kuchelewa kwingine ni kujaribu kujiridhisha kwamba hakuna udanganyifu, kuna mtu anakata bima kampuni tofauti na anapeleka madai kote kote, kitu ambacho ni kinyume na taratibu za bima, pia kuna anayeunguliwa na gari kikweliii na yupo anayenyofoa spare kibao kisha akawasha kiberiti, bima haiwezi kulipa tu kwa vile umedai, lazima uchunguzi ufanyike.
Wengine hawatofautishi bima na polisi, mfano unapotakiwa kupeleka taarifa za polisi, labda ajali/tukio au ukaguzi wa gari, wakati mwingine inachukua muda kuipata, hiyo nayo mtu anaona ni usumbufu wa bima, lakini siyo. Mara nyingi ukifanikiwa kupeleka nyaraka wanazozitaka, haichelewi kihivyo.
Ushauri wangu ni kwamba tusomage sera/mkataba, na pia pale pale unaponunua bima, tupate kujua taratibu za madai.