Insha Maridadi 1: Farasi wa Magufuli Wamegoma Kunywa Maji...

Aiseee chalii sasa umeandika nini? Ndio kashalipwa. Haya faster Nenda na wewe ulipwe B7
 
Umezunguuuuka Hadi unatia huruma

Muda WA maneno murefu kama kamba umekwisha.... Go straight to the point

Unfortunately huna point kwenye hili, ungetoa suggestions

Kaput
 
Mkuu watanzania ni desturi yetu,Nyerere na ualimu wake hawakumelewa licha ya kutawala nchi miaka 27.Katunga vitabu wee vya ujamaa na kujitegemea ,Mwongozo,tujisahihishe,It can be done play your part lakini hatukujitambua,
Labda nikupe wazo tu,Tanganyika ilipata uhuru kabla ya kujitambua,na hadi leo hatujajitambua.
Ndio maanake Mwingereza alitaka atutawale miaka mingine isiopungua 70.Tatizo si Magufuli tatizo lipo nje ya box.
 
Ukweli ni kwamba, watu wengi walio serikalini ambao mzee anawateua based on their qualifications (vyeti vya darasani) ni wezi na wachora michongo ya kupiga hela. Ukiona watu wanapanga safari kupeleka ndege ulaya ili ikapakwe rangi na kuna bajeti washaweka wazi, ujue walafi ni wengi.

Sio vibaya, baba mwenye nyumba akaja na formula yake ya kuajiri watu ambao wanaweza kumsaidia ku-deliver anachotaka.

Kuna taasisi moja duniani wao katika mfumo wa kuajiri wanafuangalia Character, then Competence na mwisho Chemistry ili kupata working culture.
Tukiwa wakweli, uwezo wa mavyeti kwa wasaidizi wa JPM uko vizuri sana, hakuna anaebisha. Ila wengi wana bad character. Wengi ni wezi, wanatamani fursa ilikiwa wazi wapige hela (suala la kupaka ndege rangi ni moja ya nini baba mwenye nyumba anatuambia).
Competence ni outcome ya mtu kuwa kwenye field baada ya kupewa nafasi. JPM mwenyewe hakuwa anajulikana kabla ya Rais Mkapa kumpa nafasi 1995 ya inaibu waziri. Tokea hapo akapata fursa ya kupanda juu. Paulo Makonda mpaka sasa kuna mjadala mkubwa wa vyeti vyake, na mpaka sasa delivarables zake zina wanawafunika watu kibao wenye ma-vyeti yao.
Katika Watanzania mil 55, sio vibaya akahukua vijana mtaani maana nao ni Watanzania na wana njaa ya kuonyesha uwezo wao.'
Creativity na spirit ya kuwa industrious nayo iko chini sana kwa watu wanajivunia kuwa watumishi wa umma.
Mzee, usione vibaya kutafuta vijana wenye vision on how solve problems which are facing Tanzanians.
Kama kwenye korosho, mpaka sasa nashindwa kuelewa kwanini wizara ya fedha, viwanda na biashara wameshindwa kumfanya mzee atabasamu kwa kuona tunauza katika Global standard.
Hao wenye simu ya mzee mbona hawampi hizi ndogondogo. Kwa wale wenye simu nami mnigee, mimmegee mzee on how he should go about to maximize value ya korosho
 

Tatizo unafikiri haya ni mambo yote ya Rais; ni vizuri watu walalamikie watu wahusika. Mkimlalamikia Rais kwa kila jambo ndio mnaona kwamba Rais anatakiwa kufanya kila kitu. Suala la MO kwa mfano; ni suala la polisi siyo la Magufuli. La Saa Nane ni suala la polisi...
 
Honestly kuna Watanzania wengi sana ni wavivu wa kufikiri, kumbukeni alichosema Rais Mkapa.
Prezaa anatakiwa apate thinkers na kuwa entrust wapige kazi.

Sio kanisani tulifundishwa Yesu alikuja kwa Wayahudi, wakampotezea, ikabidi wokuvu uende kwa watu wa nje ambao waliitwa mataifa.
Kama farasi hakubali kunywa maji ili mzigo uende, huku mtaani kuna farasi wengi sana ambao wanaweza kutoa matokeo tarajali
 
Una akili kupindukia ndugu,umemjibu mtu mwingine lakini nimeelewa mimi ,nimefarijika mimi.
 
Watu wanamsukumia lawama Rais sababu kila kukicha utasikia 'tumefanya hili kwa amri ya mamlaka kutoka juu'

Basi na sisi tunapeleka lawama kwa mamlaka iliyoko juu.
Jeshi la Polisi lisingekuwa POLICCM hakika wananchi tungeliamini utendaji wake.

Hebu rudi kidogo kwenye sakata la kupigwa risasi lisu. Polisi washatuambia uchunguzi umeshindwa kuendelea sababu mashuhuda wako nje.
Lakin hapo hapo wameshindwa kutuambia hata aina ya silaha iliyotumika kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa kwenye eneo la tukio.

Ukirudi dakika chache kabla ya tukio lenyewe haswa mkuu wa nchi anatamka hadharani kabisa 'malipo ya msaliti yanajulikana'
Na hapo kashatoka kutuelezea namna Lisu alivyokuwa anaomba taarifa za Accacia kutoka kwa Mwanyika.
 
Bwawa ruba ameingia ndio maana farasi hawataki kunywa maji kwani kuingiza midomo yao bwawani ni kuhatarisha uhai wao mimi yangu macho tu
Tutaelewana tu
Nb Magufuli si bingwa wa kupiga push ups ?
Kwanini asiwatie mateke Farasi ? Thubutuuu !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good point.
 
Moja ya sababu kubwa inayomfanya Rais aendelee kufeli ni kuzungukwa na watu wanafiki ambao kazi yao kubwa ni kumsifia hata kama anaelekea shimoni,huu ni udhaifu mkubwa alioutengeneza mwenyew kwa kupenda sifa asizostahili.Ukiondoa neno Rais,John ni mtu wa kawaida na mwenye fikra za kawaida sana.Kutokana na mifumo yetu mibovu iliyoasisiwa na katiba neno Rais linamfanya aonekana exceptional yaani ana akili kuliko wote jambo ambalo halina ukweli wowote kwa sababu hakuna mahala imeandikwa kuwa Rais lazima awe na akili kuliko wote.Kutokana na sababu hizi zilizompa rais mamlaka makubwa ya kufanya lolote analotaka ndizo zinazosababisha watu wanaomzunguka wakose nguvu na hivyo kuwa opportunist kwa either kupiga vigeregere au kukaa kimya kimya mwenye nguvu afanye.
Kwa maoni yangu mleta maada ni miongoni mwa watu wanafiki either kwa kulinda maslahi binafs au uelewa mdogo katika kutambua mfumo/style za uongoz wa John.Acha kuzungukazunguka chanzo cha matatizo ni yey mwenyew kwa kuwa yupo self centred,tumeshuhudia wasaidiz wake wenye maono tofauti akiwatumbua hvyo wengine wameona bora taifa lipate hasara kuliko kupoteza nafas zao
 
Huyu Mzee Mwanakijiji mimi hua sisomi hekaya zake,kwa sababu anakera sana,nyeusi yeye husema nyeupe,hajui hata kusoma body language za watu,hawezi kutofautisha propaganda na hali halisi.Ana macho lakini haoni,ana masikio lakini hasikii.
 
Kwamba magufuli hana Siasa za chuki?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda na hao wanaolipa milioni 5 kupaka gari rangi linalogharimu milioni 7 nao wanalizwa wanahitaji kufanya ukaguzi wa ghafla!
May be, lakini hata kwa kulinganisha na bei ya kpaka rangi nyumba, hiyo 5 million inaonekana ni ndogo. Anyway., siko familiar sana na bei za Bongo.

Lakini Kitendo cha Rais kuacha kazi na kwenda kukagua maendeleo ya project/kazi ya million 5 inatakiwa kuangaliwa kwa jicho la Tatu.
 
Wataalamu wa ndege hebu watuambie kuhusu suala la Rangi, hivi zile rangi za ndege huwa ni rangi tu au kuna engineering aspect nyingi zinazingatiwa maana ninavyofahamu kule angani kuna hali tofauti sana na huku hivyo kila kiendacho kule lazima kuwe na calculations za kitaalamu ili mambo yaende sawa. TUJITAHIDI KUFIKIRI JAMANI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…