Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Nchini Rwanda kuna falsafa muhimu sana inayotumiwa kumaanisha kiwango cha juu kabisa cha Uzalendo na kuwalinda Wananchi na maslahi yao.
Falsafa hiyo inapatikana kwenye neno Inkotanyi. Neno hili linamaanisha nguvu ya pamoja inayofanywa kwa ujasiri ili kulinda Wananchi na kusimamia maslahi mapana ya Wananchi na Taifa lao.
Falsafa hii ndiyo iliyotumiwa na vikosi vilivyoongoza na Meja Generali Paul Kagame katika kuikomboa Rwanda na kuijenga upya kwa nguvu baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.
Kupitia falsafa hii, Wanajeshi wazalendo chini ya Meja Generali Paul Kagame walifanikiwa kuwaondoa Viongozi madhalimu waliokuwa wanawagawa wananchi kwa misingi ya kikabila huku wakijinufaisha binafsi kwa ufisadi wa kutisha.
Kupitia falsafa hii kikundi kile cha Wanajeshi kimefanikiwa leo hii kuunda Jeshi bora kabisa la Wananchi la Rwanda na Taasisi bora kabisa za Ulinzi nchini Rwanda. Taasisi hizi za nchini Rwanda sasa zinasifika na kuogopeka kwa kiwango cha kutisha kabisa hapa Afrika.
Wameweza kuzuia Ugaidi nchini Msumbiji, wameweza kulituliza Taifa la Afrika ya Kati na sasa wamefanikiwa kuikamata Kongo Mashariki na kuviondoa vikosi vya Mafisadi wa SADC waliokuwa wanaongozwa na JWTZ.
Falsafa hii imefanya Rwanda kuijenga vizuri na kwa kasi sana nchi yao huku wakijenga taasisi imara, kuzuia rushwa kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi pamoja na kuwa na rasilimali chache sana.
Kwa yanayoendelea nchini Tanzania, hatuna budi kulikomboa hili Taifa na kuunda upya majeshi yetu huku tukibadili muundo wake na kuwafundisha falsafa ya Inkotanyi ili yajifunze kusimamia maslahi ya Wananchi na kuwalinda Wananchi muda wote.
Falsafa hii sio tu itafanikisha kujenga uzalendo wa kweli bali pia kuyafanya Majeshi yetu kutotumiwa na vikundi vya Viongozi mafisadi wanaokandamiza wananchi ili wawatawale kwa nguvu