Lekundayo2
Member
- Nov 23, 2017
- 33
- 37
Mimi ni baba wa watoto wanne mama tofauti tofauti na niliowapata nilipokuwa kwenye harakati za kutafuta mchumba ili awe mke wangu kwenye historia yangu niliwahi kuwa na mwanamke niliempenda sana na kumpa kila kitu ambacho nilikuwa na uwezo nacho,watu wote waliotujua walijua nampenda mwanamke huyu, kama ilivyo mapenzi unaempenda akupend..huyu mtu alinitenda kwa kila namna na tuliachana kishingo upande na nikaanza mahusiano mapya.
Nilimpata mdada wa kabilaletu,huyu dada alinizidi umri kidogo lakini alikuwa mwanamke mwenye kumaanisha na sijui niseme ni ubaya auzuri ni kwamba wazazi wangu walimpenda sana tena mnoo, lakini ukweli uliokuwa moyoni mimi nilianzisha mahusiano nae sii kwa kuwa nilimpenda bali ni ili kumsaau yule alienitenda.
Binafsi nilijitaidi kuonyesha nipo nae lkn mawazo na fikra zangu zoote zilikuwa kwa yule mwanamke wa zamani, niliendelea nae lakini sikuwahi kumjali japo yeye alinijali sana ,matukio ya mimi kuwa na mahusiano na wanawake wengine hayakuisha japo sii ya kunifumania ready handed lakini yalikuwa mengi sana, tulisuluhisha na kuisha lakini shetani huwa sikuzote ukimlea lazima akuaibishe kwani siku ya siku pale nilipokuwa naishi waliona nimezidi kuleta mabint mara kwa mara pale.
Ndipo siku nimeingiza tuu mwanamke majirani wakamwambia nae akaja kunifumania live..nduo ilikuwa mara ya kwanza ya fumanizi na mwisho wa mahusiano yetu . Nilijitaidi kumuomba lakini kwa zaidu ya miaka miwili haikuwezekana adi alipokuja kumpata mchumba wake na nasikia wameshatoleana mahari..changamoto ziliendeleq za mahusiano lakini kuna siku nilichati na mdada niliejuana nae kipindi cha nyuma na hatukuwahi kuingia kwenye mahusiano na tuliamua kuanzisha mahusiano baada ya kuona umri unasogea.... dada huyu alikuwa na maisha yake ya wastani aliajiriwa nami wakati huo sikuwa na ajira, nilikuwa nabangaza.
Kwa kuwa nilipokuwa naishi kodi ilikaribia kuisha na sikuwa na uakika wa kazi basi tulizungumza na huyu mwanamke nikaamia kwake ..yeye aliishi mkoa mwingine na tukaanza maisha .mwanamke huyu alikuwa na watoto wawili wa kiume pamoja na kuwa nao sikujali kwani kwenye kama nilivyoeleza hapo nyuma niliwahi kuwa na mahusiano na mabint kadhaa na kupata watoto wanne hivyo niliona sii tatizo kuendelea kuwa nae na tumeendelea kuishi kama wapenzi hadi leo nikiwachukulia hawa watoto wake kama wangu, ingawa hadi leo ni mwaka na sijapata kazi nakula kwa nguvu za huyu mwanamke.
Kilichonifanya niwaletee hii thread ni kwamba Wazazi kule hawajui kama nina mwanamke na baba yangu alikataa kata kata mimi nisiije kuoa mwanamke wa kabila lingine, huyu sikuwahi kumpeleka kwa baba yangu kwa kuwa najua kabisa hawezi kumkubali... umri wangu umesogea nina 35 sasahivi....Nimejikuta njia panda kwa mengi, kwanza nitampelekaje kwetu huyu mwanamke wakati kabisa haitajiki sii tuu kwa sababu ni kabila tofauti pia kabila hilo ni kabila ambalo uko kwetu linapigwa marufuku kuliko kabila nyingine ndivyo nilivyokutauko kwenye kaya yetu.
Wana JamiiForums naomba mnifungue akili imefunga..sijui la kufanya, mzazi hapo alipo anasisitiza mimi kwenda uko makwetu kutafuta mchumba na nioe. Mzee huwa anasema yupo tayari kunisaidia kupata mwanamke...baba yangu ni wale wazee wakoloni mnoo wakishilia jambo hawabadiliki lkn pia ndugu zangu waliooa wanawake wa makabila mengine wamekuwa hawafanyi vizuri sana wamekuwa na kasoro za mara kwa mara ndio maana yeye amekazia sitakiwi kuoa nje ya kabila langu.
Mwanamke wangu huyu nilienae Sii kwamba ni mzuri sana kwa sura kama mwale wa awali na wala sii mwema sana kuliko wengine niliowahi kuwa nao ila ni vile sasa tumeshapitia mengie na kujuana vema, ndie mwanamke wa kwanza kuishi nae mwaka mzima hivyo na nikiangalia umri nao unaenda na ana ujauzito, kweli nitoke tena niende kumtafuta mwanamke mwingine kijijini nimuache kwa kuwa ni wa kabila langu tuu kama wazazi wanavyotaka ama nifanye nini..namuonea huruma sana huyu dada amejitoa mno kwangu amevumilia kasoro zangu nyingi pia amejitaidi kunibadilisha kitabia sana...mimi hapa nimebaki njia panda naomba mnishauri kwani mzazi wangu ni yule asielewa jambo lolote.