Ingekuwa mimi ningefanya hivi........

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Ndugu zanguni habari!

Nimekuwa nikisoma threads mbalimbali humu katika forum hii yenye kuelimisha. Mengi yamekuwa yakiongelewa kuhusu disappointments ambazo watanzania tumepata baada ya Mkuu wetu wa nchi kushika uongozi. Ni dhahiri kabisa kuwa wengi tulikuwa na matumainmi makubwa sana kuhusu utendaji wake na ndio maana akapata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi uliopita.

Mengi tumeyashuhudia katika kipindi hiki cha miaka mitano ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Mengi mazuri amefanya na pia amekosea mengine.

Nikajiwa na wazo kama leo hii Mkuu anakujia kwako na kukwambia kuwa 'Nimeamua kukuteua wewe kuwa rais wa nchi hii kwa kipindi cha miaka mitano ijayo'

Ni mambo gani ambayo yamekuwepo katika uongozi huu ungeyabadilisha au kuyaondoa?
 
miaka 5 ya kikwete haijaisha,
wewe una lengo gani? unamtetea?
twambie wewe ugefanya nini?

mengi mazuri ya kikwete yapi alofanya?
hebu angalia kushoto kwako unaona nini hapo?
tumempa nchi ameshindwa, hotuba ya jana imejaa porojo, tangu mwanzo hadi mwisho neno ni moja ''mtikisiko wa uchumi''
hana jipya,
kwa hoja yako, akija kwangu na kunichagua kuwa rais:la kwanza kushughulikia ni kumfungulia mashtaka kwa kutowajibika kwa wananchi wake,
 
miaka 5 ya kikwete haijaisha,
wewe una lengo gani? unamtetea?
twambie wewe ugefanya nini?

mengi mazuri ya kikwete yapi alofanya?
hebu angalia kushoto kwako unaona nini hapo?
tumempa nchi ameshindwa, hotuba ya jana imejaa porojo, tangu mwanzo hadi mwisho neno ni moja ''mtikisiko wa uchumi''
hana jipya,
kwa hoja yako, akija kwangu na kunichagua kuwa rais:la kwanza kushughulikia ni kumfungulia mashtaka kwa kutowajibika kwa wananchi wake,

Ndugu hatugombani!!

Umesema kazi kashindwa wewe ungeiweza?

At least umesema ambacho ungekifanya- kumfungulia mashtaka kwa kutowajibika kwa wananchi wake.

Mimi ningepitisha sheria ya kuwafunga maisha fisadiz wote nchini tena mimi ningekuwa jaji mwenyewe.
 
Mi ningeanzia kwenye kuandika katiba yetu ambayo kwa sasa imejaa viraka, na baadhi ya mambo yaliyomo humo yamepitwa na wakati.
Pili, ngingeweka mawaziri vijana wenye uchungu na nchi na wenye nguvu ya kuchapa kazi kama power tiller
Tatu, ningeweka mkazo kwenye mapinduzi ya kilimo kwani asilimia kubwa ya wananchi wanaishi vijijini na wanashughulika na kilimo. Hali ya vijijini kwa njia ya kilimo ikinyanyuka ndipo tunaweza kuona hata dalili za maisha bora kwa kila mtanzania.
Walau ningeanza na hayo!
 
Swali ni: je, taifa limeweza kupiga hatua mbele, limebaki palepale au limerudi nyuma kwa ujumla au katika sector zipi tangia JMK kuchukua nchi?
Au ni kwa vile matarajio yetu yalikuwa makubwa kupita kiasi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom