jikuTech
JF-Expert Member
- Apr 9, 2023
- 228
- 290
MALENGO YA AU MAFANIKIO YA UJUZI WA PROGRAMMING
Miongoni mwa malengo au mafanikio anayotarajia mtu anayejihusisha na programming ni kutengeneza programu za kompyuta kwa matakwa yake mbalimbali.Na ili utengeneze programu ya kompyuta lazima ujifunze lugha za programu kulingana na malengo yako.
PROGRAMMING AND SOFTWARE
Programming ndio mchakato unaoleta Software hii iko wazi.Wakati wa kutengeneza Software, Programmer anatakiwa kutafakari mambo mawili ya muhimu, User Interface, na Backend Processing.
User Interface
User Interface ni sehemu ya programu ambayo mtumiaji ambaye hawezi na haelewi kuhusu programming na mchakato mzima jinsi program inavyofanya kazi anapata uwezo wa kutumia program bila shida kutokana na maelekezo yanayo kuwepo kwenye screen akiwa amewasha program mfano. Sign in, See More, Like, share, Read More, Play, Downloand, inakuwa ni vitu ambavyo mtumiaji anaelewa kabisa kwamba nikibonyeza hapa naenda kufanya hivi. Hiyo ni sehemu ya User Interface sehemu ya program kwa upande wamtumiaji.Kuhusiana na User interface kama haujaelewa vizuri unaweza tafuta mtu anaye elewa kipengele hiki akakuelewesha zaidi ya hapa.
Backend Processing
Ni sehemu ya program ambayo michakato ya kuwezesha kazi kusudiwa ya software inachakatwa , mfano sasa mtumiaji amebonyeza Download Now basi kwenye Backend kuna kuwa na mazingira yanayo wezesha mchakato anao utaka mtumiaji kwa wakati huo , wa kudownload kile alicho kiona na kukipata kama alivyokusudia. Mfano user anataka ku log in kwenye backend ndio sehemu pekee ambapo taarifa zina linganishwa kama ni sahihi na kutoa ruhusa au kukataa ombi la mtumiaji. Mbinu ya kujifunza zaidi kitu ni kutafuta taarifa zake nyingi, kwa hiyo hapa nilikuwa najaribu kutoa mwanga ila unaweza kufuatilia zaidi kwenye masomo ya Backend Programming.Data / Taarifa
Programming inafanya kazi na taarifa, software ina tegemea taarifa ili iziendeshe kwa namna mbalimbali kama alivyo panga mtengenezaji kwa software yake itaenda kutatua changamoto gani . Katika Programming kuna Utaratibu wa kuhifadhi taarifa.Taarifa huhifadhiwa kwenye Database, Kuchakatwa kwenye Server na kisha Mtumiajia.
Mtumiaji anapo jisajili kwenye mfumo flani anakuwa anawasiliana na server ifanye kazi anayo ikusudia mfano kujisajili anakuwa anaiambia server imsajili, ambapo server itachukua taarifa za mtumiaji huyo na kisha kuzihifadhi kwenye database kwa ajili ya baadaye zikihitajika ziwepo.
Mtumiaji anapo Log in anawasiliana na server, server inafanya uchunguzi kama hizi taarifa zipo kwenye database au amna kama amna ina kata ombi kama zipo inatoa ujumbe wa OK na taarifa zinazohitaji kwa mtumiaji huyo.
Taarifa zinaweza kuwa za aina nyingi mfano, Video, Maneno, Picha na Audio. Server inafanya kazi kwa kushirikiana na database ili kutoa huduma kwa mtumiaji, yaani inapokea maombi na kujibu kama ilivyo elekezwa na aliye itengeneza. Ambaye kwa wakati huo utakuwa wewe.
User Interface Technology / Frontend Programming
Kabla sija taja chochote naweza toa dokezo kidogo hapa kama hauja wahi kujifunza programming nakushauli uanze na HTML uje CSS kisha JAVASCRIPT hii ni mwanzo mzuri wa kuelewa jinsi Software inavyo fanya kazi kwa upande wa mtumiaji, nazungumzia software kwa sababu lengo sio kuishia kuwa programmer lengo kubwa ni ku kutengeneza Software za uhalisia.Jifunze Lugha hiyo kwa mpangilio huo hapo juu, jinsi ya kuanza unaweza tafuta sehemu yoyote ambayo kuna mafundisho ya hizo vitu, ukimaliza hapo utakuwa na uelewa wa Sehemu ya Mtumiaji kwenye Programu. Usiogope kuomba msaada kwa mtu baada ya kuwa umesha anza tayari, Jinsi ya kuomba msaada usijaribu kuomba msaada kwa mtu ukiwa hauja aanza kujifunza kwani utaishia kujidhalilisha kwa kuwa hautaelewa hata cha kuuliza anza kujifunza tumia juhudi ukikwama tafuta iyo changamoto kwa kutumia AI na Google na sehemu zingine kisha usipo lizika ruhusa sasa kuuliza kwa mtu mwenyewe ana uzoefu.
Ukisha kuwa umejifunza kwa usahihi mambo hapo juu, Tafuta Frameworks mbalimbali za kupendezesha Frontend yako.
Zingatia frontend niliyo itaja hapo juu ni utangulizi wa kuelewa nini maaana ya UI kwa ujumla yaani inahusika na nini katika programming na nimeshauli ujifunze hayo kwa sababu kwenye taaluma hii hakuna namna ya kujifunza kwa kusoma maelezo zote ni kufanya kwa vitendo ndio uelewa unakujia kusoma unaweza soma maelezo yote , unaweza skia maelezo yote pia lakini usielewe kuelewa ni kujifunza kwa kufanya , wengine wanajidanganya kwamba kujifunza hayo mpaka uwe na kompyuta kitu ambacho kama Uchumi hauruhusu kwa wakati huo ni kigumu na unaweza kujifunza kwa kutumia simu yako ila iwe smartphone, zipo program online za kuandika code za kujifunzia na kuzi run na kupata matokeo kwa kutumia simu, Yaani naamaanisha kuna safari ambayo computer sio lazima ndio kuna mahali ukifika unahitaji computer tena kuitumia tu unakuwa unaweza hata bila kuelekezwa kutokana na mafunzo yako ya awali.
Backend Technology / Programming
Kasi yako ya kujifunza ndio inayoweza fanya usonge mbele zaidi lakini haraka haisaidii labda kuelewa tu. Katika sehemu hii utatakiwa kujifunza lugha za programu zitakazo kusaidia ku kufahamu utendaji kazi wa software katika sehemu ya program kwa awali ni kisema kwa awali maana yake kuna zaidi yapo ukisha Jifunza nitakacho sema hapa. Ili kuendana na sehemu ya mtumiaji kama nilivyo sema hapo juu unatakiwa kujifunza teknolojia hizi kwa mpangilio wa kuanza na PHP kisha MYSQL, PHP inafanya kazi katika server ni kama processor ndani ya server, wakati huo MYSQL ni lugha ya kuwasiliana na DATABASE kutoka kwenye Server.Hii hii ya lugha mbili (2) kwa mtu anaye anza inakamilisha mchakato au dhamila ya Software katika kufanya kazi na taarifa, mtumiaji anatuma maagizo ama ya kupeleka taarifa zichakatwe yaje majibu au ya kutuma taarifa zihifadhiwe kwa ajili ya baadaye au maagizo ya kutuma taarifa zihifadhiwe katika DATABASE.
PHP, kama unaanza jifunze tu jinsi ya kufanya kazi ya kutengeneza API za
ku-CREATE (POST),
ku- READ (GET),
ku-UPDATE(UPDATE) na
ku-DELETE(DELETE)
php ni lugha pana sana lakini kwa kuanza jifunze namna ya kufanya hivyo na PHP kwa sababu ya dhumuni la kufahamu utendeji kazi wa software kwenye backend vingine baada ya kufahamu elimu hii utaona mwenyewe vinapanda ukigusa tu unakuwa unaelewa sana.
MYSQL, kwa mwanzoni hapa lugha hii ni pana pia ila unatakiwa kujifunza jinsi ya
ku-INSERT,
ku-SELECT,
ku-SET,
ku-DELETE
Baada ya hapa Mtu utakuwa na uwezo wa kukaa na kufikilia uhalisia wa tatizo Fulani na kuwazia jinsi software inavyoweza kuwa. Hivyo hadi hapa una kuwa na uwezo wa kutengeneza mifumo kama programmer kwa kiwango cha kati, suala la upo kiwango cha kati wewe mwenyewe ukijifunza hadi hapo utaelewa unako takiwa kufika bila kuambiwa na mtu.
Elimu hii hadi hapa Ni ufunguo wa kuwa Full Stack Developer
Utakiwa kujifunza kuhusiana na Ujasilimali wa Mtandao ili uweze kujipatia pesa kidogo kabla hauja endelea mbele kwenye kukamilisha taaluma yako ya kuwa software engineer.
........................................................................................................
Jiku Tech Tips inajivunia kuwa mshirika wako katika safari yako ya kujifunza na kukuza ujuzi wa teknolojia. Kama Full Stack Developer mwenye uzoefu na Mkufunzi mtaalamu, Jiku Tech Tips imejitolea kukupa mafunzo bora na yenye tija katika ngazi zote:
- Ngazi ya Awali: Tunaweka msingi imara kwa wanaoanza, tukihakikisha unaelewa dhana za msingi za programu na teknolojia.
- Ngazi ya Kati: Tunakusaidia kukuza ujuzi wako zaidi, kukufundisha mbinu za hali ya juu na kukupa uwezo wa kutatua changamoto za kikazi.
- Ngazi ya Juu: Tunakuandaa kuwa mtaalamu wa teknolojia, kukufundisha kuhusu mifumo changamano na kukupa ujuzi wa kuongoza miradi ya teknolojia.
- Uzoefu wa Kina: Tunajua mahitaji ya soko la teknolojia na tunakupa mafunzo yanayokufaa.
- Mbinu Shirikishi: Tunatumia mbinu za kufundisha zinazokushirikisha kikamilifu, kuhakikisha unaelewa na unakuwa na uwezo wa kutumia ujuzi ulioupata.
- Mtaala Uliopangwa: Tuna mtaala uliopangwa vizuri ambao unakusaidia kujifunza kwa utaratibu na kufikia malengo yako.
- Msaada Endelevu: Tunakupa msaada wa kutosha hata baada ya mafunzo, kuhakikisha unaendelea kukua na kufanikiwa katika taaluma yako.
Tembelea kiungo hiki hapa chini kuingia kwenye mafundisho ya IT -TEHAMA yanayo endelea mtandaoni kupitia WhatsApp,Youtube na Live Session
<<<< Jifunze Information Technology (IT-TEHAMA) >>>> au
Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja