jikuTech
JF-Expert Member
- Apr 9, 2023
- 228
- 290
AINA ZA KOMPYUTA
Aina za kompyuta zinaweza kuelezewa kwa namna mbili kulingana na ukubwa pamoja na uwezo wa kuchakata taarifa kama ifuatavyoAina Za Kompyuta Kulingana Na Uchakataji Wa Data
Analogue KompyutaDigital Kompyuta
Hybrid Kompyuta
Analogue Kompyuta
Hizi ni kompyuta ambazo utendaji kazi wake ni wa moja kwa moja yaani inavokuwa inachukua data ni zinatumika zilizo ivo ivo amna kuchakatwa tofauti na aina zingine za Kompyuta ambazo taarifa lazima zibadilishwe kuwa binary data na kisha kuchakatwa mfano wa Kompyuta hizi ni Speedometers na Mercury Thermometer.
Digital Kompyuta
Hizi ni Kompyuta ambazo zimeundwa mahususi kwa ajili ya ku-perform calculation na logical operation kwa speed ya hali ya juu. Yenyewe inachukua taarifa kwa mfumo wa binary yaa 0 na 1 na kuzichakata kwa kutumia programu ambazo zinakuwa zimehifadhiwa ndani ya Kompyuta
Mfano wa komputer hizi ni zile zote za kisasa kama vile laptops na desktop Kompyuta pamoja na simu janja (smartphone)
Hybrid Kompyuta
Hizi ni kompyuta ambazo zina namna kama analogue na digital Kompyuta yaani zina Speed kama analogue Kompyuta na zina ufanisi kama digital Kompyuta kompyuta hizi mara nyingi zina tumika hospitalini , kwenye ndege na kwenye maswala mazito ya utafiti wa kisayansi.
Aina Za Kompyuta Kulingana Na Ukubwa
SuperKompyutaMainframe Kompyuta
Mini Kompyuta
Workstation Kompyuta
Personal Kompyuta
SuperKompyuta
Hii ni aina ya Kompyuta ambayo imeundwa kwa namna ya kuchakata ma trillion ya taarifa kwa sekunde moja tu kompyuta kama hizi mara nyingi zinakuwepo ofisi za hali ya hewa kwa ajili ya utabili wa hali ya hewa . Zingatia hii Kompyuta inaweza kuchakata ma trillion ya taarifa kwa sekunde moja tu. Utengenezaji wa siraha za nyukilia unategemea Kompyuta ya aina hii, masoko ya hisa yanategemea Kompyuta hizi ungozaji wa satellite unategemea Kompyuta hizi
Mainframe Kompyuta.
Hii ni Kompyuta ambayo imeundwa kwa uwezo wa kutumiwa na ma elfu ya watu kwa wakati mmoja , kompyuta hii inauwezo wa ku run maelfu ya program tendaji kwa wakati mmoja na kwa ufanisi na mantiki hii ndio inawezesha utendaji rafiki kwenye mashirika ya Bank na Mitandao ya Simu Telecom organization Ndani ya bank inarecord ma million ya miamala kwa wakati mmoja , ndani ya Telecom Org ina wezesha mamillion ya miunganiko ya mawasiliano kwa wakati mmoja.
MiniKompyuta
Hii ni aina ya kompyuta ambayo ni kama mdogo wa mainframe ambayo yenyewe inakuwa na uwezo wa kutumiwa na watu kuanzia wa nne hadi mia mbili ( 4-200) kwa wakati mmoja na mara nyingi hutumika kwenye mataasisi na department kwa ajili ya masuala ya fedha na mahesabu ya fedha hii ni Kompyuta ambayo inakuwa na uwezo na ukubwa ambao ni kati ya mainframe na microKompyuta
Workstation Kompyuta
Hii ni Kompyuta yenye uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja, microprocessor yake inakuwa na speed kubwa pia inakuwa na RAM kubwa na mara nyingi Kompyuta hizi huundwa kwa ajili ya kazi flani maalum mfano graphics workstation, music workstation au engineering workstation.
Personal Kompyuta/MicroKompyuta
Hii ni Kompyuta ambayo imeundwa kwa namna ya kuwa na matumizi mengi na ni kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja mmoja. Laptops na Desktop Kompyuta zote kwa pamoja ni microKompyuta.
Hadi hapa mjadala wa aina za Kompyuta unakuwa umeisha, kwa mujibu wa andiko hili lakini pia kuna mahala unaweza kuwa hauja elewa jambo ambalo sio la kuwa na wasiwasi kabisa kwa maana safari bado inaendelea ya kujifunza Kompyuta kwa undani kuna maneno yameandikwa yanaweza kukuchanganya lakini usijali mda sio mwingi utakuwa na ufahamu nayo.
Pia baada ya kujifunza matumizi ya mtandao katika kurasa zijazo utakuwa na uwezo wa kufuatilia jambo lolote kwa undani kwa kutumia kivinjali na injini ya utafutaji View 07
Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja