Information Technology(IT-TEHAMA)-05

Information Technology(IT-TEHAMA)-05

jikuTech

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2023
Posts
228
Reaction score
290

AINA ZA UJUZI WA KOMPYUTA​

Ujuzi wa kompyuta kwa upana unaweza kusemwa kwa namna mbili

Moja ujuzi wa kimsingi
Pili Ujuzi wa kitaalamu

Ujuzi wa kimsingi:​

Ujuzi huu anahitaji mtu yoyote anaye taka kutumia Kompyuta kwa matumizi madogo madogo kama vile kutuma barua pepe, kutumia mitandao ya kijamii, utafutaji wa taarifa mtandaoni na kukamilisha taarifa mbalimbali za kiofisi.
Huu ni baadhi ya ujuzi muhimu katika ujuzi wa kimsingi wa Kompyuta
Kuendesha Mifumo endeshi ya Kompyuta kwa ufanisi mfano Windows na MacOs kwa maana ya kufungua na kufunga program mbalimbali , Kutengeneza na Kutunza Files pamoja na Kurekebisha mipangilio mbalimbali ya Kompyuta

Kutumia Program za kuchakata documents/nyaraka kama vide program ya Microsoft Office ambayo hutumika kuandaa nyaraka mbalimbali kama vile maandiko ya ofisini, barua, na repoti

Kutumia ujumbe wa kielectronic emails, mtu ataweza kutuma na kufungua email zinazo ingia katika kifaa chake. Ataweza kutuma files na viambatanisho vya picha,video,docs nk

Kuvijari kwa kutumia vivinjali kama vile Google Chrome na Firefox Mozilla ambazo hutumika kufungua internet katika kifaa kwa ajili ya kutafuta taarifa mtandaoni kupitia wavuti na kujaza fomu mbalimbali mtandaoni.

Kutumia Mitandao ya kijamii, kama vile Facebook, Twitter, LinkedIn katika kufanya mahusiano (networking), Masoko na Mawasiliano.

Ujuzi Wa Kitaalam/ Ujuzi Wa Hali Ya Juu kwenye tehama​

Huu ni ujuzi/taaluma maalamu ambao ni kwa ajili ya jambo maalam na ujuzi wenyewe unahusisha maarifa ya juu ya software program, Lugha mbalimbali za Kompyuta na mifumo mbalimbali ya Kompyuta yaan complex Kompyuta systems

Hapa ni mifano ya ujuzi wa juu wa Kompyuta

Programming: hii ina husisha kunadika code kwa kutumia lugha za Kompyuta kama vile Java, C, C++, Python nk ujuzi wa juu katika kipengele hiki no pamoja na utengenezaji wa Complex Algorithm na Application mbalimbali,. Unaweza ukawa hauelewi kinacho zungumziwa hapa kwa sasa ila kwa mbele utapata picha kamili..

Web Development: Hii ni taaluma ya kutengeneza wavuti mbalimbali kama unavyo ona www.bongoclass.com hii ni tovuti ya kitanzania inayo jihusisha na elimu katika masuala mbalimbali ya kijamii na kitechnolojia.

Graphics design:

Data analysis:

View 06

Bonyeza HAPA Ingia kwenye mafunzo haya, Ujifunze moja kwa moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom