Inflation vs Deflation kipi kina afadhali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Inflation vs Deflation kipi kina afadhali?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pianist, Apr 29, 2012.

 1. Pianist

  Pianist JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Hizi dhana mbili za inflation(mfumuko wa bei/kupanda kwa gharama za maisha (kutokana na ongezeko la fedha)) na deflation(punguzo la jumla ya fedha zitumiwazo ili kudhibiti bei) zimekuwa zikinichanganya(mimi sio mchumi) kujua ipi ni afadhali katika uchumi wa nchi kama yetu.  Inflation inasaidia taasisi za fedha kudhibiti uchumi katika mikopo na riba, pia hufanya watu waweze kutumia pesa zao pindi wanapozipata wakihofia bei kupanda kila kukicha, pia waajiri huweza kuongeza mishahara kwa mfano inflation ni 10% na mwajiri anaongeza mshahara kwa 5%. Inflation huweza kuwekeza pesa zao kuliko kuzihifadhi kusubiria thamani yake ipande. Athari hasi za inflation ni pamoja na kusababisha watu wadai malipo zaidi ya bidhaa wanazouza au ujuzi/nguvukazi wanayotoa, pia watu huweza kununua bidhaa na ‘kuzivundika’ kusubiria thamani ya hizo bidhaa ipande, maandamano makubwa yanaweza kutokea kutokana na bidhaa kupanda kama nchi jirani watu walipoandamana kupinga kupanda kwa bei ya mkate,

  Kwa upande wake deflation inapunguza bei za bidhaa, inaongeza nguvu ya ununuzi wa bidhaa zinunulikazo kwa pesa, inasaidia wale wenye vipato visivyobadilika. Lakini deflation husababisha watu wasiwekeze pesa zao na badala yake ‘wazivundike’ kwani thamani ya pesa inapanda kila kukicha. Kibaya ni kwamba deflation huleta ‘deflationary spiral’ yaani: Bei zimeshuka, wazalishaji/makampuni/waajiri wanapata faida ndogo kutokana na mauzo ya bidhaa kwa bei rahisi, hivyo inabidi wafanyakazi wapunguzwe, wasio na kazi wanaongezeka wakiwa hawana pesa ya kutumia, wazalishaji/makampuni/waajiri inabidi wapunguze zaidi bidhaa kwani wanunuzi wamepungua zaidi na bei zinazidi kupungua zaidi. Ikifika hapa taasisi za fedha hazina cha kufanya kwani huwezi kuweka riba yenye viwango hasi(negative interest rate). Si rahisi kwa waajiri kupunguza mishahara, hakuna anayependa kupunguziwa kipato chake.


  Je kipi ni bora Inflation au Deflation
   
Loading...