Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 299,623
- 752,057
Inferiority complex ni hali ya kujikataa, hali ya kujiona si bora kuliko wengine.. Inferiority complex ni kinyume cha superiority complex.
Watu wenye tatizo hili hupenda;
- Kutafuta kuungwa mkono hata kwa jambo la kijinga na kipumbavu kabisa
- Hupenda kujistukia hata kwa vitu vidogo kabisa
- Hupenda kujikataa kujitenga na kususa hata kwa vitu ambavyo havina uzito wowote
- Ni wepesi kulaumu wengine hata mahali pasipostahili lawama
- Ni waoga mno wa kukosea
Inferiority complex ni kizalia pia ni makuzi , kuna watu wamezaliwa bila hili tatizo lakini makuzi na malezi toka kwa wazazi na walezi wakawasababishia hili tatizo kikubwa kikiwa ni mateso na kunyanyaswa kulikopitiliza.
Lakini kuna ambao wamezaliwa nalo lakini kwa kupata wataaalam wanaweza kumsaidia mtu kupunguza hili tatizo.
Kimsingi hakuna haja ya kujilinganisha na wengine, Jifunze kuwa wewe... Tuache mitazamo ya kuamini kwamba tofauti zetu za kimaisha na kimitazamo zinatufanya bora au dhoofu mbele ya wengine.
Hakuna anayeweza kukufanya inferior bila wewe mwenyewe kutaka... Inferiority complex can be cured.