GE2025 INEC yamuita Mpina kurejesha fomu ya Urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imepanga kupokea fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais na Makamu wa Rais kupitia Chama cha ACT Wazalendo siku ya Jumamosi, Septemba 13, 2025, saa nne asubuhi, katika ofisi za tume jijini Dar es Salaam. Wagombea waliopendekezwa na chama hicho ni Luhaga Mpina na Fatma Fereji

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi, Juma Rahisi kwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu na ambayo Jambo TV imeithibitisha, wagombea wanatakiwa kuzingatia masharti ya Kanuni ya 20(4) ya Kanuni za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani za mwaka 2025

Miongoni mwa masharti hayo ni kuwasilisha fomu zilizojazwa kikamilifu, picha nne za rangi zenye mandhari meupe, uthibitisho wa malipo ya dhamana ya Shilingi milioni moja, na fomu namba 10 ya tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi

Tume imeelekeza kuwa kila mgombea ataruhusiwa kuambatana na watu wasiozidi kumi (10) pekee, bila shamrashamra au maandamano ndani au nje ya jengo la tume

Hatua hii inajiri siku moja baada ya Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma, kutoa uamuzi kwamba Mpina ana haki ya kuendelea na mchakato wa kurejesha fomu ya kugombea Urais wa Tanzania

Katika shauri Na. 21692/2025, Mahakama ilibainisha kuwa zuio lililowekwa na INEC Agosti 27, 2025, kwa kumzuia Mpina kurejesha fomu, lilikuwa kinyume cha sheria na Katiba

Uamuzi huo, uliotolewa Septemba 11, 2025 na Jaji Abdi Kagomba, ulieleza kuwa waleta maombi- Bodi ya Wadhamini wa ACT Wazalendo na Luhaga Mpina walikuwa na haki ya kupewa nafasi ya kurejesha fomu kwa wakati. Hata hivyo, ombi lao la kulipwa fidia ya Shilingi milioni 100 lilikataliwa



Chanzo: Jambo TV
 
Kwa vitendo, kwa muonekano, "Tume Huru" ya Taifa ya Uchaguzi, haiko huru na wala haisimamii uchaguzi kwa weledi unaotazamiwa.
Kesi hii ya Mahakama imewaumbua sana.
Heri wangeitwa tu Tume ya Serikali ya Uchaguzi.
 
Kwa hiyo baada ya fomu kupokelewa ndo barua ya msajili itakuja kwa ajili ya pingamizi na mambo yanaishia hapo kwamba mgombea hana sifa?
 
Kwa vitendo, kwa muonekano, "Tume Huru" ya Taifa ya Uchaguzi, haiko huru na wala haisimamii uchaguzi kwa weledi unaotazamiwa.
Kesi hii ya Mahakama imewaumbua sana.
Heri wangeitwa tu Tume ya Serikali ya Uchaguzi.
Walikaa miezi kadhaa kutafuta neno "HURU" likae wapi. Walipokosa wakaamua kuondoa neno TAIFA wakaweka HURU
 
Huu ndiyo Uchaguzi wa kuwadanganya Wazungu kwamba ni huru ili watupe Mikopo?

Waseme wazi kwamba hii Nchi ni ya Chama kimoja kuliko haya maigizo yao
Haya maigizo soma hapa yalivyoandaliwa


 
Walikaa miezi kadhaa kutafuta neno "HURU" likae wapi. Walipokosa wakaamua kuondoa neno TAIFA wakaweka HURU
Hii Nchi tuna safari ndefu sana, sijui miaka 50 ijayo hali ya Siasa itakuwaje kama tumeanza kunajisi Vyombo vya maamuzi kiasi hiki Kwa manufaa ya upande mmoja 🙌
 
Tuna hali mbaya sana kama Taifa 🙌
 
Kwa vitendo, kwa muonekano, "Tume Huru" ya Taifa ya Uchaguzi, haiko huru na wala haisimamii uchaguzi kwa weledi unaotazamiwa.
Kesi hii ya Mahakama imewaumbua sana.
Heri wangeitwa tu Tume ya Serikali ya Uchaguzi.
Ingeitwa Tume ya CCM ya Uchaguzi. Ni aibu tupu. Eti retired Judge wa Mahakama ya Rufaa ndiyo mwenyekiti wa hiyo tume… Bullshit!
 
This has got to be the worst script ever written.

Hapo kilaza ajuza anajikuta bonge la genius.
 
Tume huru 🤔🤔🚶🚶🚶🚶
 
Ole wake ingekua ni CDM ingekua ndo imeisha hiyooo!!!
 
Aibu sana kwa tume inayoongozwa na manguli wa sheria, majaji wastaafu. Sasa walizitolea wapi guts za kuwakataa kina Mpina na Fatma Fereji? Hii si tume huru abadani
 
Hii haina hadhi ya kuitwa Tume huru ya uchaguzi, labda ingeitwa Genge la Wahuni la Kuhadaa Uchaguzi.
 
Asa mbona yeye atakuwa amechdlewa kuanza kampeni au atafidiwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…