INEC yafafanua mchakato pingamizi na rufaa za udiwani

INEC yafafanua mchakato pingamizi na rufaa za udiwani

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 53 na 65 vya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka 2024, baada ya uteuzi kufanyika, wagombea wa Ubunge na Udiwani wanaruhusiwa kuweka pingamizi dhidi ya uteuzi.

Soma pia: INEC yawaita wagombea ubunge, udiwani kuchukua fomu

Screenshot 2025-09-01 023736.png


Rufaa Zilizokubaliwa

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, rufaa mbili za wagombea udiwani zimekubaliwa. Wagombea hao ni:

Yasini Mazoea Bakiri, mgombea udiwani Kata ya Mlingula, Jimbo la Ndanda kupitia ACT-Wazalendo dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda.

Alex Tresiford Nachingulu, mgombea udiwani Kata ya Mwena, Jimbo la Ndanda kupitia ACT-Wazalendo dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ndanda.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, wagombea hao wamerejeshwa katika orodha ya wagombea udiwani katika kata husika na wanaruhusiwa kuendelea na taratibu za kampeni za uchaguzi.

Rufaa Zilizokataliwa

Hata hivyo, rufaa tatu za wagombea udiwani zilikataliwa. Wagombea hao ni:

Abisai Raston Hankungwe, mgombea udiwani Kata ya Mabatini, Jimbo la Mbeya Mjini kupitia CHAUMMA, dhidi ya Stephen Kael Mwaisumo, mgombea udiwani Kata ya Mabatini kupitia CCM.

Mwajuma Hamidu Tito, mgombea udiwani Kata ya Nanganga, Jimbo la Ndanda kupitia CUF, dhidi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Nanganga, Jimbo la Ndanda.

Jacob Jaston Mdolo, mgombea udiwani Kata ya Ilolo, Jimbo la Vwawa kupitia CCM, dhidi ya Richard Mwendanjila Kibona, mgombea udiwani Kata ya Ilolo kupitia CHAUMMA.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, kwa wagombea namba (i) na (ii), Tume imekubaliana na maamuzi ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa kata husika wa kutowateua kugombea nafasi ya udiwani.
 
Back
Top Bottom