GE2025 INEC yaahirisha uchaguzi Fuoni, sababu ni kifo cha mgombea Abbas Mwinyi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
1758885304711.jpeg

Kutokana na kifo cha mgombea ubunge wa Fuoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Ali Mwinyi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeahirisha uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo hadi pale itakapopanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea.

Abbas ambaye ni kaka mkubwa wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, alifariki dunia jana Septemba 25, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 25, 2025 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Fuoni, Miraji Mwadini Haji, amepokea barua kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kuhusu taarifa ya kifo cha Abbas.

Amesema kutokana na kutokea kwa tukio hilo, uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Fuoni lililopo Wilaya ya Magharibi B- Zanzibar, umesitishwa kuanzia Septemba 25, 2025.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 71(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 1 ya mwaka 2024, Tume kwa notisi itakayochapishwa katika gazeti la Serikali itapanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea na taratibu za uchaguzi wa ubunge katika jimbo husika zitaanza upya.

“Hivyo, uteuzi kwa wagombea wengine ambao walioteuliwa kihalali utabaki kama ulivyokuwa awali, isipokuwa kama mgombea atajitoa na kwamba hakutakuwa na kampeni kwa wagombea ubunge katika Jimbo la Fuoni mpaka baada ya uteuzi wa mgombea mwingine,” inaeleza taarifa hiyo.

Pia Soma: TANZIA - Abbas Mwinyi Mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi afariki dunia

1758867988311.png
 
Kuliko kuahirisha yule aliyeshika nafasi ya pili angeingia mzigoni tu hata kama imebaki mwezi mmoja watamchagua. Hii ni kukwepa gharama mpya
 
Natamani hiki kifo kisiishie kwa huyu tu!, KWA KUWA KIFO NI KIFO TU....Isiishie ngazi ya UBUNGE TU!....HUU MFULIZO WA VIFO VYA WAGOMBEA NA UENDELEE HIVI HIVI! KWA JINA LA ALIE JUU...AMINA!.
 
Mbona kafanana sana na samia kuliko hata huyo hussein.! Nilijua Labda kaka wa sa kafa
 
Eulogy (Tribute)

The evolution of president kids.

Huyu muungwana enzi za utoto wetu, tulikuwa na uwanja wa mpira ‘siew view’ kati ya Gymkhana Golf Club na bahari ilipo (sina uhakika kama lile eneo leo halina mgorofa).

Na miaka hiyo mpira tulikuwa tunacheza watoto wa ‘siew view’, upanga na wengineo wenye talent popote wanapotekea.

Kocha akiwa ‘Tade Shelukindo’ japo Abbas akiwa mtoto wa kishua (matter of fact zama hizo kujiona mtoto wa kishua ni kama aibu).

Tade alikuwa mshikaji sana na Abbas.

Abbas alikuwa akitoka magogoni kwa miguu kila jioni anamfuata Tade kuona sisi wadogo zake tunapocheza mpira.

Wenyewe Tade na Abbas wapo juu kwenye kilima fulani hivi wame chill, jamaa hana hata mlinzi hata mmoja.

Na watoto wanaotoka mbali yeye na Tade wana walipia nauli kutoka mfukoni kwao.

Tukimaliza mazoezi ya mpira, Tade anamsindikiza nusu safari. Hakuna mtu alikuwa anamuogopa mtoto wa raisi miaka hiyo.

Leo hii watoto, wa raisi watakaa saangapi na watoto wa maskini, let alone kuona sote ni binadamu sawa.

Abbas Mwinyi was very normal ujanani.

R.I.P
 
Huko si wana ZEC?!! Why INEC ndiyo itoe taarifa?

Halafu huko hakuna wabunge ni wajumbe wa baraza la wawakilishi?
 
Kutokana na kifo cha mgombea ubunge wa Fuoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Abbas Ali Mwinyi, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imeahirisha uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo hadi pale itakapopanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea.

Abbas ambaye ni kaka mkubwa wa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi, alifariki dunia jana Septemba 25, 2025 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Lumumba iliyopo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 25, 2025 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Fuoni, Miraji Mwadini Haji, amepokea barua kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kuhusu taarifa ya kifo cha Abbas.

Amesema kutokana na kutokea kwa tukio hilo, uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Fuoni lililopo Wilaya ya Magharibi B- Zanzibar, umesitishwa kuanzia Septemba 25, 2025.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 71(2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba 1 ya mwaka 2024, Tume kwa notisi itakayochapishwa katika gazeti la Serikali itapanga tarehe nyingine ya uteuzi wa wagombea na taratibu za uchaguzi wa ubunge katika jimbo husika zitaanza upya.

“Hivyo, uteuzi kwa wagombea wengine ambao walioteuliwa kihalali utabaki kama ulivyokuwa awali, isipokuwa kama mgombea atajitoa na kwamba hakutakuwa na kampeni kwa wagombea ubunge katika Jimbo la Fuoni mpaka baada ya uteuzi wa mgombea mwingine,” inaeleza taarifa hiyo.

Pia Soma: TANZIA - Abbas Mwinyi Mtoto wa mstaafu Marehemu Ali Hassan Mwinyi afariki dunia
Nilifikiri ingekuwa bora wakaupiga chini wote.
 
Huko si wana ZEC?!! Why INEC ndiyo itoe taarifa?

Halafu huko hakuna wabunge ni wajumbe wa baraza la wawakilishi?
ZEC inasimamia uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi. INEC inasimamia uchaguzi wa Wabunge. Marehemu alikuwa ni mgombea Ubunge na si Uwakilishi. Au hufahamu kuwa kwenye Bunge la URT huwa kuna wabunge kutoka Zanzibar?
 
Najua wapo,alikuwa akiwachachafya Ally Kessi wa Nkasi pale bungeni.

Ila nilifikiri hao wabunge kutoka Zanzibar wote hupatikana kwa usimamizi wa ZEC yao halafu chama chao ndiyo kina-appoint wa kuja Dodoma!
 
Back
Top Bottom