India wanawabagua waafrica

India wanawabagua waafrica

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
26,683
Reaction score
59,181
Magazeti ya leo yamereport kwamba india wanawabagua waafrica. Waandishi hawajaelezea uhusuano kati ya wahindi wanao ishi tanzania na waafrica wa tanzania.
 
Na kwa Africa wahindi wanajibagua hawachanganyikani na waafrika.
 
hahahahahaha huku wanapewa hadi ubunge..godamn it
 
hivi kuna wabunge na viongozi wa serikali watanzania huko India wangapi?
 
serikali ya ccm imeshindwa kulazimisha ushirikano miongoni mwa wahindi na watanzania. wanataka watu tusiseme ubaguzi wa wahindi na dharau zao. wanataka tusiseme hiyo hali kwamba italeta ubaguzi. basi wawakemee. mia
 
Wahindi wenyewe kwa wenyewe wanabaguana sembuse Mhindi na Mwafrika?
 
Wahindi wenyewe kwa wenyewe wanabaguana sembuse Mhindi na Mwafrika?

Wewe kweli unawajua wahindi,hawa jamaa ni wabaguzi hatari,niko nao kama 20 nafanya nao kazi hawaishi kupigana majungu hawa
 
Magazeti ya leo yamereport kwamba india wanawabagua waafrica. Waandishi hawajaelezea uhusuano kati ya wahindi wanao ishi tanzania na waafrica wa tanzania.

Hakuna sehemu isiyo na ubaguzi!
Btw, India hata wao kwa wao wanabaguana!
 
Magazeti ya leo yamereport kwamba india wanawabagua waafrica. Waandishi hawajaelezea uhusuano kati ya wahindi wanao ishi tanzania na waafrica wa tanzania.
Chanzo mkuu!!
But all in all nenda pale coco beach uone ubaguzi wao hawa shwaini!
 
hawa watu hata kwenye movie zao bado wanaonyesha ubaguzi. niliona movie moja ambayo ndo kwa mara ya kwanza na muona mwafrika, sikupenda character yake hata kidogo. Alikuwepo model ambaye alikuwa ameanza kushuka daraja so akawa mlevi usiku mmoja kaenda dico afu akamuopoa jamaa wa kiafrika akalala naye. Huyo dada asubuhi yake alikuwa akilia wakati anajisugua bafuni. Huyo mwafrika mwenyewe hakuongea hata kidogo. i hated it.
 
Hakuna sehemu isiyo na ubaguzi!
Btw, India hata wao kwa wao wanabaguana!

India kuna matabaka tena makubwa ya wao kwa wao, na tabaka linalodharauliwa zaidi na ambali ni maskini zaidi ni kutoka South India. South India ndipo wanapopatikana wahindi weusi, ndio maskini sana kule sub continent ya India. Miji ya Mumbai, Delhi Amritsar, Hyderabadi kuna ubaguzi sana ambapo huwezi kwenda kutembea kwenye maeneo ya wakubwa na utajishtukia kama si kutemwa mate.

Kwenye miji kama Gujarat na sehemu zingine kama Qadian, kule walau kuna usawa zaidi maana kuna muingiliano wa dini kidogo na imesaidia maana utakuta waislam na wakristo wanapatikana.

Ukiwakuta wahindi wenyewe ambao ni Hindu wanaoabudu kwenye srinigar, au wale wenye imani ya masingasinga...huko ni 100% ubaguzi.

Kutokana na over population ya India, toka mwanzoni mwa miaka ya 1900 wahindi wengi walihama kwao na kukimbilia nchi za Afrika ambapo walizaliana, wakapata watoto, wakapata wajukuu na wamesalia kuwa ni raia halisi tena kwa kuzaliwa. Kitu ambacho sisi waafrika hatukuweza kulikimbia bara hili na kwenda kutafuta makazi/maisha kwao India. Ndio maana mpaka leo hii, tunao viongozi ambao wana asili ya India kama vile Prof Issa Shivji etc.
 
Kaka umeeleza vizuri ila nikurekebishe hapo uliposema South India ndio wanaongoza kwa umaskini,SI KWELI,mimi nipo Bangalore(IT city of India) na moja ya miji inayokua kwa kasi India,miji mingine ya South ni Chennai(Industrial Hub of India due to large port),hydrebad na Kerala(state with largest educated people who scattered all over the world),na hapa Bangalore ni moja ya majiji yenye wageni wengi sana hususan wa Africa wanaokuja kusoma,pia wahindi wengine wanaotoka North(hususani Chinks....wanaofanana na wachina wanatokea Assam,Sikim n.k).
Pia ukiangalia states kama Jarkhandi,Bihar,Rajahstan na Sikkim,ni maskin sana.
Uzuri wa huku kusini ubaguzi si mkubwa sana sababu zikiwa ni pamoja na kuwepo kwa wakristu,waislam wengi pia elimu imewasaidia maana watu wamepata exposure kama ya kwenda US,UK,Dubai na sababu kubwa ni IT companies kama INFOSYS na WIPRO ambazo headquarters zao zipo hapa Bangalore.
Ila pia sio siri ubaguzi bado upo,mfano mim mwenyewe nina rafiki yangu msichana,tukiwa tunaongozana barabarani utaona vijana wanatukana au wanamkashifu huyo dada.
Pia kwaupande mwingine sisi wenyewe waafrika tunachangia unakuta watu wana fanya after parties mpaka saa nane za usiku wakibughuzi watu waliolala,wasichana wanavaa nusu uchi kabisa ambapo huko nyumbani wasingethubutu,pia watu kama wanigeria wanajihusisha na biashara harama kama kuiba kwa kutumia debit cards,drugs n,k.
 
Naomba mjadala usiwe na mwelekeo wa kuleta ubaguzi mwingine hapa....nchini...maana tuliyonayo bado haijapatiwa ufumbuzi wa maana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom