India: Ukuta waanguka na kuwauwa wageni 22 kwenye harusi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
248275d3f9b4344eb8e9204d00caab73.jpg
Takriban watu 22 wamefariki baada ya ukuta kuwaangukia wakati wa harusi Kaskazini mwa India

Wageni hao walikuwa wamejikinga na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kabla ya ukuta huo kuwaangukia

Watu wengine 26 wakijeruhiwa katika ajali hiyo ya Bharatpur, wilaya moja ya jimbo la Rajasthan, 15 kati yao wakiwa na majeraha mabaya

Vyombo vya habari vinasema kuwa vibanda vya kuuza chakula vilikuwa vimewekwa kandokando ya ukuta huo karibu na harusi

Ukuta huo na ulianguka kutokana na kimbunga kulingana na Afisa wa Polisi Anil Tank aliyenukuliwa akisema


Alisema kwamba ukuta huo wenye urefu wa futi 90 uliwaangukia wageni wengi

Waliojeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali za eneo hilo mara moja huku wakipewa matibabu.

Chanzo: BBC
 
india matukio ya vifo vingi kwa pamoja ni vingi sana,cjui ni nini?
Miundombinu yao ni ya kizamani imechoka mfano ukiangalia hata ajali ya Treni huwa inasababisha maelfu kupoteza kufariki.!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom