Inawezekana!!

Mundali

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
749
164
ELIMU, AFYA, MAJI, UMEME (BURE AMA KWA GHARAMA NAFUU VIPO NDANI YA UWEZO WETU)

Wana JF na watz kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwaletea mada hii tuijadili. Kwa mtazamo wangu upatikanaji wa elimu na afya bila gharama yoyote ni suala ambalo lipo ndani kabisa ya uwezo wa nchi yetu. Kinachokosekana ni utashi pekee.

Serikali yetu imeshindwa kukusanya kodi na hivyo kushindwa kutoa huduma hizo kwa jamii. Kukusanya kodi ni jambo la kitaalam na linalohitaji ubunifu wa hali ya juu, kwani wlipa kodi kila kukicha huamka na mbinu mpya za kukwepa kodi. Sasa ukizingatia uhalisia wa serikali yetu, na kukithiri kwa rushwa nchini, utaona jinsi kodi inavyokusanywa kiasi kidogo sana, huku mzigo mzito wakiangushiwa wafanyakazi wa sekta rasmi.

Nitoe mfano mdogo tu jinsi tunavyokosa mapato. Natumai kila mmoja wetu kwa namna moja ama nyingine anatumia mawasiliano ya simu za mkononi. Na kila unaponunua muda wa hewani unalipa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) 18%. Katika kila sh. 100 unayotumia shs. 15.25 (Sh. 100 inajumuisha VAT) inakuwa ni VAT (pesa ya serikali).

Kuna watumiaji waliosajiliwa wapatao milioni 9. Iwapo kwa siku hao watumiaji milioni 9 wanatumia shilingi 100, serikali inapaswa kupata sh. 137,250,000/- kwa mwezi 4,117,500,000/-. Hapo tunaweza kukusanya zaidi na zaidi iwapo tu serikali itakusanya kodi toka kwenye chanzo (tax at source), na si mfumo uliopo (tax on invoice). Yaani wakati makampuni ya simu yanapomkata mteja anapopiga simu na serikali ipate kodi yake palepale (kuweka mtandao unaofanya kazi sambamba na mitambo ya makampuni ya simu).

Hiyo ni changamoto moja tu, lakini tunamaeneo mengi sana yanayoweza kuifanya nchi hii kuwa na surplus budget. Bila kusahau Tanzania ni Dubai ya ukanda huu, naishia hapo, naomba michango yenu.
 
Economics ingekuwa nyepesi kiasi hicho, basi nyote humu mngekuwa na PhD kwenye uchumi. :becky:
 
Economics ingekuwa nyepesi kiasi hicho, basi nyote humu mngekuwa na PhD kwenye uchumi. :becky:

Ukiweza kurudisha pesa zilizoibiwa na makampuni tata ya Richmond,meremeta,tangold,stewart, pesa za EPA,misamaha ya kodi ya mzee wa hekima wa Rombo 11 B basi unaweza kujenga zahanati kila ward hapa Tanzania na ukaongeza ajira kwa watanzania.,simple Economics
Just like you ignore it....
But you must accept the reality.....
ccm cannot do it.............
wameweka pesa kule visiwa vya chenge..............
watasubiri kipindi cha uchaguzi wafanyie kampeni...............
Huu ni ukweli bana muulize Malaria sugu.................
 
Economics is avery simple subject tought in complicated minds. Economics starts at your home. Problem of economists of our country uses statistics which contravenes with day to day life style of our people. Changamoto ndogo: How one can measure our National Income in correct way (Tanzania)?
 
Ushauli huu nadhani unatakiwa uzingatiwe na vyama vyoote vya siasa, chama chochote kitakachoshinda kifanye haya.
Tuipende nchi yetu tusiwaachie wachina, wamarekani, wahindi, wakenya, waganda n.k kutuendeshea nchi yetu.
Raisi atakayeshinda akae na tupange maendeleo yetu, misaada haitatufikisha popote, tuache uvivu tufanye kazi kila mtu alipo afanye kwa bidii zote, mafisadi, rushwa na wenye tamaa mwisho uwe sasa.
 
Tathmini hii ni nzuri na ya Ki tanzania na inaonyesha kwamba wapenda nchi hawajapotea wakati walanchi wakiongezeka, big up!!
 
Back
Top Bottom