Mara nyingi wanaume wanachukulia " Mfupa uliomshinda fisi mimi nitauweza?" lakini nadhani hii ni mtazamo tu. Wewe jaribu kujitambua kuwa una nafasi gani kama mwanamke kitu ambacho wengi kinawashinda, kuwa na watoto sidhani kama ni kipingamizi labda uwe nao wengi kiasi cha kuathiri uchumi wako na huyo atakayekupenda kukuoa. Ushauri, unatakiwa ujipende, ujielimishe sio lazima darasani ujue ulimwengu unaendeleaje na usiwe mvivu wa kufikiri kiasi kwamba mtu akiongea na wewe u-synchronise naye.