wanasheria tunaomba mtushauri kwa maana jambo la watu waliojenga mabondeni limeachwa kuwa ni makosa yao na hivyo kuonekana hawana stahili yoyote.
Binafsi naamini inawezekana watu hawa kulipwa fidia. Wengi wanasema sheria ziko wazi na kama hawa hawajui sheria basi sheria zinatamka wazi kuwa kutokujua sheria si sababu ya kuhalalisha kuvunja sheria.
Mimi nadhani mpaka watu hawa wamejenga mabondeni kuna uzembe umefanyika. Je, ni nani kafanya uzembe? Na huyo aliyefanya uzembe ndiye ana wajibu wa kubeba mzigo huu.
Je, kazi ya serikali ni kuchukua sheria na kuzifungia kisha kuangalia waliovunja sheria? Au kazi ya serikali ni kuwaongoza wananchi kwa kuwaelekeza hapa panafaa kwa matumizi haya au pale hapafai kwa matumizi haya na yale?
Kimsingi hapa tunaangalia kama kodi za Watanzania zitumike kuwalipa waliojenga mabondeni fidia au zikafanye kazi ya kujenga miradi ya maendeleo. Lakini kama kuwalipa wananchi hawa fidia inaweza kuwa fundisho kubwa kwa serikali kutambua wajibu wao na kujua wao pengine ndio wa kutuhumiwa kwanza inaweza kutusaidia zaidi.
Tunataka serikali iwe mbele yetu ikituonyesha njia na sio kuwa nyuma yetu ikiangalia nani kakosea wakati hakuna aliyetangulia kuonyesha njia ni hii.