Inawezekana vipi mtu akajiajiri ambapo hajawahi kuuza hata karanga? Serikali acheni porojo, toeni ajira kwa wahitimu

Mtu na nusu

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
636
1,115
Kichwa cha habari kinajieleza vizuri.

Hizi story za kujiajiri ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya viongozi wa serikali ambao wao ni waajiriwa zinaumiza sana.

Haiwezekani nipo shuleni kuanzia Nina umri wa miaka 6 Mpaka leo Nina miaka 25/26 then uje uniambie nijiajiri.

Najiajiri Nini Sasa?

Inaudhi sana.
 
We ni tatizo kabisa ktk nchi hii.

Kila mwaka vyuo vinatoa wahitimu,unadhani ajira za kuwatosha wote zinatoka wapi ktk nchi hizi za kiafrika masikini?

Unapaswa kujiongeza kwa akili ya kuzaliwa kwamba juhudi zako hazitegemei mawazo ya wengine wawaze cha kufanya ili wakuajiri wewe ,unapoambiwa tegemea akili yako,juhudi na maarifa ndiyo tafisiri ya neno "KUJIAJIRI "

Kaa hapo unasubiri serikali utakufa masikini
 
Cha kushangaza wao wanapishana na mav8 kuroga ili wabakie hapo na hawataki kuja kujiajiri ili kupisha hizo nafasi wakae wengine
🀣🀣🀣🀣🀣Mungu anawaona
Utasikia sijui kamatia fursa yani tunawazoom tu,
 
Cha kushangaza wao wanapishana na mav8 kuroga ili wabakie hapo na hawataki kuja kujiajiri ili kupisha hizo nafasi wakae wengine
Mungu anawaona
Utasikia sijui kamatia fursa yani tunawazoom tu,
So ndo hapo.
Inashangaza Kuna watu wanawasapoti humu

Hakuna mtu anaweza kujiajiri bila sapoti
Watoe basi hata mitaji
 


Hawa ndo unakuta wanatembea na bahasha halafu nauli wanapewa na wadogo zao wanao uza maji au kutengeneza makochi..
Wao akili zao zote ni kuajiriwa na kulaumu serikali...
 
Hawa ndo unakuta wanatembea na bahasha halafu nauli wanapewa na wadogo zao wanao uza maji au kutengeneza makochi..
Wao akili zao zote ni kuajiriwa na kulaumu serikali...
Anadai serikali iwape mitaji..anapewa yule anayeonesha nia kweli...lol...
 
natamani kutoa darasa na kwa mifano tena kwa vijana yaani tuanze nadharia kisha vitendo nauhakika nikiwa na vijana 50 baada ya miezi sita tunaweza kuwa sehemu fulani na baada ya miaka miwili 25% wanaweza kumiliki biashara zao wenyewe ikiwemo 10% walioajiri watu wawili kila mmoja.
 
Yes walitakiwa watoe hata mtaji na sio maneno tu,,

Mtaji gani mnataka wakati shule mmeenda na nguvu mnazo?

Hamuwaoni wenzenu hawajaenda shule lakini wanaosha Tu miguu wakina dada na kukunja hadi 150k kila siku??

Wewe why usijiunge huko?

Wanaouza maji mitaani huwaoni?
Unajua wanaigiza ngapi kwa siku?

Nikikwambia ajira unayoitafuta mshahara wake hautafika hata nusu
Ya wanachopata waosha miguu
Utaamini?
 
Id yako thou🀫πŸ˜ͺ
 
Kwahio mkuu wengine waliojiajiri hawakupita shule kama wewe?
Wewe hukwenda kujiajiri kwa kukosa option, you went there because you chosen that path! Wanaolalamika hapa ni hawa ambao waliambiwa soma mwanangu upate kazi nzuri πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… akili imejengwa hivyo toka ground β€œ0” halafu ghafla unaambiwa kazi amna jiajiri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…