Thorin Oakenshield
Member
- Apr 6, 2015
- 36
- 15
Nimewahi kusikia kutoka kwa watu wangu wa karibu, ndugu na jamaaa waliowahi kufanya kazi ama wanaofanya kazi kwa wahindi hadi hivi sasa kuwa, kama mfanyakazi ukionekana una mawazo chanya, mwenye akili nyingi, mjanja na mvumbuzi wa mambo kiasi ambacho unaweza kumshauri bosi nini mfanye kwa ajili ya maendeleo ya kampuni basi unaweza kuishia kufukuzwa kazi kwani jamaa hao (yani wahindi) huwa wanahisi kuwa kwa akili nyingi ulizonazo huenda ukawa unawapiga kiaina bila wao kujua. Kwahiyo ili kuendelea kufanya kazi kwenye taasisi zao ni bora kujifanya mjinga tu au zoba ili kulinda ajira yako.
Sasa kwenye kaya yetu, watu wengi wanasema mkuu wetu hashauriki hata kidogo. Wazo likanijia, huenda anashaurika na washauri wapo wengi wenye akili nyingi tu na mawazo ambayo yataisongesha mbele kaya yetu sema wanaogopa kutoa huo ushauri na kuamua kukaa kimya ili waendelee kupata chochote kitu kwa ajili ya mkono kwenda kinywani maana utumbuaji umekuwa wa hali ya juu. Hii inapelekea mkuu kuwa 'One man army' na kufanya maamuzi mengi makubwa kama ambavyo akili yake inamtuma bila kuhojiwa ama kushauriwa na yoyote yule.
Karibuni wadau tujadili.