haiwezekan kwasababu subwoofer nyingi hasa hizi za kichina mfumo wake wa kusoma usb ni wa moja kwa moja yaani kama unachomeka flash pale au memory card kupitia card reader basi subwoofer ile ina connect moja kwa moja kupitia njia nne ambazo ni +vcc, gnd clock na data.
hivyo simu mara nyingi ukikonect ktk vifaa kama vile computer au baadhi ya dvd kunakuwa na option ya kuruhusu mass storage itumike yaani memory. sasa subwoofer hazina option hiyo ya kuifanya simu ikuletee sehemu ya kuruhusu mass storage
cha kufanya tafuta waya wa audio utoe sauti kutoka kwenye simu iingie kwenye subwoofer kupitia audio input then badilisha input ktk subwoofer yako mpaka utakapo fika katika input ulio ingizia audio