Inawezekana akawa ana mimba au nachezewa akili tu?

Lavit

JF-Expert Member
May 16, 2011
13,464
28,068
Wadau poleni na mihangaiko ya maisha.

Kwa kifupi nilikuwa nadate na binti mmoja kabla hajahama kwenda mkoa mwingine, mara ya mwisho nimelala naye Jan 3 ya mwaka huu Jan 4 aliniambia yupo siku zake na kiuono kinamuuma sana, baada ya situation hiyo kulitokea sintofahamu mpaka anaondoka.

Sasa leo kanitumia sms ananiambia ana ujauzito wangu, nimemuuliza imewezekana vipi apate mimba yangu wakati baada ya kukutana na mimi uliingia katika siku zako.

Amejibu hata yeye hajui, ila amepima kaambiwa ana mimba ya miezi miwili na hajakutana na mwanaume mwingine zaidi yangu.Nikaona isiwe kesi, nikamwambia sawa itabidi azae tu, cha ajabu ananiambia eti hayuko tayari kuzaa kwa sasa.

Wadau bado simuelewi huyu binti, kwanini akazanie kutoa. Je ni njia tu ya kunidanganya.
 
Anakazania kutoa kwa sababu hayuko tayari kuzaa sababu anazijua yeye zinaweza kuwa,ana mwanaume mwingine,hataki kuzaa na wewe as haoni future na wewe,ana matatizo ya kiafya au kifedha,ana vipaumbele vingine kwenye maisha au hajatulia tu kuwa mama sasa. Kazi kwako kama mwanaume kumshauri na kuonyesha una nia si tu ya kupata huyo mtoto bali hata kumtunza na yeye na kuwa na ndoa nae...mimba sio kitu kirahisi kukubaliana nacho kama hujajipanga.
 
Michelle

Mkuu unajua mazingira ya mimba yana utata, kingine nilikuwa na malengo naye ila yeye hapa mwishoni ndiye amebadilika!!
 
Last edited by a moderator:
Anataka Pesa, Mchezo Huo Tunafanya Sana Wadada, Sema Tu Amekosea Gia

ndiyo maana nimehoji hiyo mimba imeingiaje ameishia kupanick eti kwa hiyo mimba kajipa mwenyewe?
 
gwankaja

Sasa mkuu kama mazingira yana utata kwanini unataka kubeba huo mzigo ambao unasaidiwa kuuondoa? Katika vitu najua vinafurahisha wanawake ni mwanaume ambaye amekupa ujauzito na unampenda na amekubali mtoto azaliwe na yuko tayari kutunza mtoto na unaona ana huo uwezo.

Ukiona mwanamke pamoja na utata hataki kuzaa jua tu kuna kubwa zaidi ya hilo ndani ya moyo wake. Amebadilika ana sababu mkuu....mpe muda,si ana akili zake au ulikuwa na mtu asiyejua zuri na baya.
 
Last edited by a moderator:
Mwambie azae tu..kutoa dhambi.. Hata hivo its impossible aingie MP then awe na ujauzito..
 
Toa hela, watu wana shida, inaonekana wewe ni bahili sana, sasa katumia mbinu hiyo, maana hapo hamna mimba kuna kirungu tu.
 
Mwambie azae tu..kutoa dhambi.. Hata hivo its impossible aingie MP then awe na ujauzito..

Its possible kuingia P ukiwa pregnant,especially kipindi cha mwanzo.kuna hizo cases.
Girl anaeza shangilia kapata P ila baada ya mwez anagundua she is pregnant.
How?siwezi kuelezea kitaalam.ila kuna walotoa shuhuda imewatokea
 
Inawezekana kwa mwanamke kupata siku zake akiwa na mimba. Kama bado unamshuku basi saidia pesa ya clinic akizaliwa mtoto fanya dna test.
 
Back
Top Bottom