Inawezakana CDF na IGP wakapiga salute kwa mkuu wa Wilaya?

Mkuu wa Wilaya ni muwakilishi wa rais,

So,hiyo ni heshima kwa muwakilishi wa rais kwenye wilaya.
CDF wala IGP hapashwi kumpigia salute mkuu wa wilaya, kwa IGP PGO inamtaka kumpigia salute kuanzia RC, hapo CDF hajapiga salute bali kapokea salute na ndo sababu unaona yuko mguu pande.
 
CDF wala IGP hapashwi kumpigia salute mkuu wa wilaya, kwa IGP PGO inamtaka kumpigia salute kuanzia RC, hapo CDF hajapiga salute bali kapokea salute na ndo sababu unaona yuko mguu pande.
PGO gani hiyo inayomkataa mkuu wa wilaya kisha inampitisha RC???

wote kiutendaji wanazidiwa majukumu na IGP achia mbali CDF,kinachohalalisha wao kupigiwa salute ni uwakilishi wao kiutendaji kwa rais wa jamhuri.

ukiwa ndani ya wilaya basi boss mwakirishi wa rais ni dc,ukiwa mkoani ni rc.
 
CDF mwakilish wa nani?na nani Yuko karibu na kiti kati ya CDF na DC,km kaipokea ni sawa lkn CDF kumsalute DC haiwezekani.
cdf sio mwakirishi wa rais.cdf ni cdf.

mbali na kwamba cdf huonekana karibu zaidi na rais kuliko mtumishi mwingine,lakini kuna barrier kubwa sana ya mazungumzo ya kiutendaji,tofauti na DC au RC kwa rais.
 
Kila nikiangalia hii picha nashawishika kuuliza hivi ni nani mkubwa kati ya hawa wawili kivyeo na mamlaka View attachment 2255912
kwakweli licha ya wote ni wateule wa rais lakini mkuu wa majeshi kwa mwono wangu ni mkubwa sana.Moja kitaluma ya jeshi,pia ni mkuu ktk majeshi ya nchi hapo unaona mapana yake halafu et ampigiye salut mkuu wa wilaya,mkoa.Heri ingekuwa wazir mkuu au spika tu.
 
Naomba nijibu kama ifuatavyo:

Kuu zinaongozwa na sheria ya National security council act ya mwaka 2010 namba 8.

Ambayo inatoa mwongozo ya muundo wa Baraza hili linavyoundwa.
Inatoa pia mwongozo vyombo vinavyohusika
Ingawa ls.4 inasema Baraza linaweza mwita mtu yoyote mwenye hujuzi wa kitu muhimu kwa huo wakati.

Vyombo vinavyohusika ni:
Jeshi la wananchi wa Tanzania
Jeshi la polisi Tanzania
Jeshi la Uhamiaji Tanzania
Idara ya usalama wa Taifa
Mshauri wa Mgambo.
Jeshi la Magereza Tanzania.

Muundo kwa Ngazi ya Kitaifa

Raisi JMT
Makamu wa raisi JMT
Raisi wa Zanzibar
Waziri Mkuu
Katibu Mkuu kiongozi

Na sekretarieti kutoka Majeshi ya Tanzania.

Kumbuka hii ndio hatua juu ya kimahamuzi katika Taifa hili.

Labda unavyofikiri hapo mkuu wa wilaya ana nafasi?
View attachment 2254808View attachment 2254809

According to the Order of Seniority

I) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
II) Mhe Makamu wa Rais wa JMT
III) Mhe Rais wa Zanzibar
Iv) Waziri Mkuu
V) Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar
Vi) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Vii) MHE Speaker wa JMT
VIII) Jaji Mkuu
 
Back
Top Bottom