Uchaguzi 2020 Inavyoonesha CHADEMA na ACT-Wazalendo hawataungana. Nini kimekwamisha?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,834
18,835
Baada ya kumuona Membe amechukua fomu ya Urais leo, nimehitimisha hakuna kuungana Kati ya Chadema na ACT licha ya vyama hivyo kupigia debe suala hili kabla hata ya mchakato wa uchaguzi

Nilitarajia Chadema kuwaachia ACT majimbo yote Zanzibar na Urais na majimbo ya ukanda wa Pwani ambako CUF ilikuwa na nguvu kabla ya kumeguka, na ACT walipe fadhila kwa kuinga mkono CHADEMA kwenye Urais wa Muungano

Nilimsikia Mbowe na Tundu Lissu wakitamka kuwa japo wamesimamisha wagombea nchi nzima na Zanzibar walikuwa tayari kuwaondoa baadhi ya majimbo kwa Sababu walikuwa kwenye mazungumzo na ACT,

Je, ni nini kimekwamisha Muungano huu?
 
Nafikiri bado mazungumzo yanaendelea na ni vizuri kila mgombea akachukua fomu yake lakini bado yawezekana akajiondoa na kumunga mkono mgombea wa chama mshirika. Na ndivyo itakavyokuwa, msihofu.
Asante. NEC wakiweka fitina kwa Lissu, tunamuunga mkono Membe hata kwa super glue. Lazima kila mmoja achukue form ili tujue uhuni wao.
 
Nafikiri bado mazungumzo yanaendelea na ni vizuri kila mgombea akachukua fomu yake lakini bado yawezekana akajiondoa na kumunga mkono mgombea wa chama mshirika. Na ndivyo itakavyokuwa, msihofu.
Membe keshachukua fomu, NEC watamuweka kwenye karatasi ya kura
 
Mkuu tuongee uhalisia hivi unaachiwa vipi kitu ambacho tayari una udhibiti nacho?
CDM wanawezaje kusema wana waachia ACT majimbo ya Zanzibar wakati ukweli ni kwamba wanajua hata kama CDM wakiweka mgombea wao hatamshinda wa ACT?

Bara nako CHADEMA wanasema watawaachia ACT mikoa ya pwani ambako tayari kila mtu anajua ACT au CCM watashinda.

Huu muungano ni wa kuifaidisha CDM tu kiuhalisia hasa hapo kwenye kuachiwa majimbo mengi bara na kuachiwa uraisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Muungano lazima uoneshe kila mtu anatoa kitu flani siyo yeye anapokea tu na kuongezewa alichonacho na mwenzie haongezewi kitu.

Niwashauri kama wana nia ya dhati ya kuungana basi waachiane hivyo walivyopanga lakini atakaepewa uraisi wa Jamhuri na kushinda basi ateue wabunge wote wa viti maalum vya raisi toka chama kingine kilichokubali kuachia uraisi, pia waziri mkuu atoke chama kilicho achia (kama katiba ina ruhusu) au wagawane nafasi baraza la mawaziri 50/50.

Hii kamari niliyo pendekeza ni kama tu kweli wanajiamini yupo wa kumshinda Magufuli miongoni mwao.
 
Chadema si wakuamini. Rejea yaliyotokea Jimbo la Segerea, Na majimbo ya Mkoa wa Kigoma kwenye uchaguzi mkuu 2015. ACT n chama Cha wasomi na waona mbali, hawawezi kuingizwa kingi na wasanii wa CDM
 
Chadema wahuni sana,na Zitto anajua hilo,mwaka 2015 walivifanyia ndivyo sivyo vyama walivyoshirikiana navyo,kovu lipo na tunajifunza kutokana na makosa,
Kama vipi chadema wamuachie Membe
 
Back
Top Bottom