kanali mstaafu
JF-Expert Member
- May 17, 2015
- 4,317
- 4,118
Unajikuta kijana umesoma mpka chuo kikuu peke yako katika familia ambayo hakuna hata aliye na cheti cha kudato cha nne. Umemalza masomo unajishikiza kufnya kibarua ambacho utaweza kula tu na kulipa kodi. Ila unapoangalia hali ya maisha kijijini katika familia unayotoka wazazi wana-approach to 70s na ww ndiye unategemewa huku hauna kazi maalum wala biashara.
Naomba kuweka wazi yaliyonisononesha katika msimu huu wa sikukuu. Ni baada ya bosi kugoma kutoa hela ya sikukuu kabla ya tar ya posho ambayo ni tar 4 huwa tunapokea, huku familia kijijini ikinitegemea. Nikiongea na watoto wa marehem dada yangu wana zaidi ya miez mitatu hawana hata viatu wanapekua ndipo nilipokopa na kutuma sh. Elfu kumi wanunuliwe angalau vya kuzugia sikukuu na kilichoniumiza zaid ni siku ya krismas watoto hawa nilipoongea nao kupitia cm ya bibi yao wakaniambia nyumban hawajala vizur kama familia nyingine. Leo jioni baada ya kuongea nao waliniuliza "hivi mjomba na mwaka mpya utakuwa kama krismas?" Kauli hii iliumiza moyo wangu na hasa mfukoni sikuwa hata n pesa ya kuwatumia.
Ukweli kuna muda nakaa nawaza sana juu ya wazazi wangu ambao wana-approach to 70s wakiwa na maisha magumu na wananitegemea mm mtt wa mwisho niliyesoma angalau nina dira kuliko yeyote ktk familia na hawa wazazi hawana mtt wa kuwapa hata thumni zaid yangu. Mm mtegemewa ndiye mimi ambaye hata tu kulipa kodi huwa ni vuta nikuvute. Sambamba na maisha magumu ya watoto wa marehemu dada yangu. Huwa nawaza ni nini hatima ya dhiki ktk familia yangu na je nitaweza kulibeba jahazi linalozama mm ambaye ni mtegemewa huku dira ya kupata kazi au initiative za pesa ya uhakika haisomeki??. Huwa inaniuma sana na mwisho huu wa mwaka nimeona nimalize na post ya kuzungumzia maisha yangu.
JF IMESHAKUWA NI FAMILIA YA WATU WANAOTIANA MOYO,WANAOSAIDIANA NA KUSHAURIANA na leo nimeamua ku-share na nyinyi sononeko la moyo wangu enyi ndugu zangu wa jf
HAPPY NEW YEAR.
KANALI MSTAAFU