Inauma kumpenda asiyekupenda ila kwanini uendelee kuteseka?

Crystal field theory

JF-Expert Member
Sep 16, 2014
907
342
INAUMA SANA KUMPENDA MTU ASIYEKUPENDA.

Umemtumia mtu text lakini hajakujibu, meseji imepokelewa lakini hajajihangaisha kukujibu. Ukaamua kuiweka simu pembeni kuendelea na mambo mengine baadae unarudi bado unaona kimya hajakujibu.

Lakini ukitizama Watsapp unaona yuko online busy akichati na kubadili DP na status. Unabaki ukijiuliza ana chat na nani mpaka asizione meseji zako na kuzijibu? Unabaki ukiendelea kujiuliza umemkosea nini?

Unaanza kujiambia kuwa labda amekuchoka. Inauma sana kupuuzwa na mtu umpendae kwa moyo wote.

Je unajua kuna uwezekano nae anapitia kipindi kigumu kama hicho? Sawa anaweza akakwambia anakupenda au amekumiss, lakini anae mtu mwingine ambae anampenda haswa.

Unavyohangaika kumpigia, kumtumia meseji na asizijibu nae aweza kuwa anafanyiwa hivyo na ampendae.

Anamtumia meseji, anamcall lakini nae simu zake hazipokelewi kama wewe. Nao wanapitia magumu kama wewe!

Kufikia hatua hii, unafikiri kukata tamaa juu ya huyo mtu lakini inakuwa sio rahisi. Unafikiri kumuacha huyo mtu, kumblock hata kum "unfriend" fb lakini bado unaona moyo wako bado unampenda. Na unamatumaini ipo siku atarudi.

Kila muda unapotaka kuichukua simu yako unaomba Mungu ukute meseji yake lakini ukishika tu simu unakuta meseji ya TIGO wakikukumbusha kulipa deni ulilokopa kwa ajili ya muda wa maongezi.

Unajikuta unaichukia simu yako na unamchukia kila mtu anaye kuongelesha, unatamani uipasue simu vipande vipande!

Lakini kwanini ifikie hatua hiyo? Kwa hali kama hiyo inaonesha kabisa wewe hupendwi labisa. Kwanini upoteze muda wako kumpenda mtu asiyekupenda?

Usimlazimishe akupende, wewe sio mzee kiasi kwamba huwezi kupata mtu mwingine. Usijipe stress kwa asiyekupenda kuwa na ujasiri wa kumuacha aende na wewe enenda na maisha yako.

Hata iwe vipi maisha lazima yaendelee.
 
Achana nae huyo mdogo wangu.
Muogope mtu ambae unampenda hala anachukulia poa upendo wako.

Tafuta mwanamke au msichana mwingine naamini wapo wanajua nini maana ya upendo Mkuu.

Najua inauma sana katika hali hiyo ila kwa upande mwingine inakufanya uwe imara katika mapenzi na mambo mengine Mkuu.
 
Acha kabisa,ni bora ujiambie huyo sio wako tena...hakupendi tena,kuna mtu anaempenda na kumuheshima kiasi kwamba Hata akichelewa dak.0.5 kujibu Sms yake anaumia na kuomba msamaha. Wewe anakuona unamsumbua,muache tu. Better stay with a broken heart for a while utasahau na utaanza maisha mapya bila yake. Au Ana cha dhahabu kiasi kwamba ushindwe kumuacha?
 
unasubiri ujibiwe meseji umechangia hela ya vocha?

acha waliomnunulia kifurushi cha mwezi wajibiwe we endelea kusubiri siku akipewa ofa na tigo ndio atakujibu
 
Mimi wa hivyo nawauzaga kwa watu wengine siku jamaa akifanikiwa kula mzigo anapiga simu kwangu anampa huyo dem anamwambia msalimie brother na Mimi namtajia jina langu ndipo nguvu zinamuishia
 
Acha kabisa,ni bora ujiambie huyo sio wako tena...hakupendi tena,kuna mtu anaempenda na kumuheshima kiasi kwamba Hata akichelewa dak.0.5 kujibu Sms yake anaumia na kuomba msamaha. Wewe anakuona unamsumbua,muache tu. Better stay with a broken heart for a while utasahau na utaanza maisha mapya bila yake. Au Ana cha dhahabu kiasi kwamba ushindwe kumuacha?

Hapo kweli ni kuwa na uvumilivu tuu yatapita ila name itakuja mtesa kabisa. Na chakunishanga zaidi hataki kukutamkia kuwa mapenzi naye yameisha anabakia kukuchora me hiyo Naona huyo hajui mapenzi nitamaaa zamsumbua ila itafika siku yake atakukumbuka wakati huo we unamaisha mengine tayari anakuja omba msamaha
 
Back
Top Bottom