Sitanii
JF-Expert Member
- Nov 20, 2024
- 516
- 692
Wakuu kwema?
#No Reform, No Election.
Tunaishi katika ulimwengu wenye vitu vingi, vijulikanavyo na visivyojulikana, vyenye kueleweka na vile ambavyo ni fumbo kubwa kwetu wakazi wa dunia.
Katika kuelewa kuna vingine hueleweka upesi, vingine huchukua muda mrefu na vingine havitaeleweka kabisa.
Katika miaka yangu hii ya kuishi niliyojaliwa, nimeona na kusikia baadhi ya mambo nikatafakari lakini nikaishia kusema ndivyo Ilivyo.
01. Kuna mtu/watu waliotupambania tufikie mafanikio, tulipoyakaribia Tu waliondoka duniani. Maumivu ya kusherehekea mafanikio bila uwepo wao hayapimiki.
02. Wapo watu wanatuamini Sana na tunapopitia magumu tukiona kiza kitupu mbele, tunawaambia juu ya kuachana na swala husika. Wao husema "endelea Tu, Hilo Jambo utaliweza na ushindi u karibu". Inaumiza Sana tunakosa kauli za kujitetea. Tunaaminiwa kuliko uwezo wetu.
03. Inaumiza Sana pale MTU wako wa nguvu anayekusaidia Kila ukikwama, lakini wewe unakuwa vibaya Sana pale anapohitaji msaada wako kiasi cha kushindwa kumsaidia.
04. Wapo wale tuliowaamini Sana, lakini mwishowe wakatufanyia ndivyo sivyo (naongelea mambo ya utafutaji)
05. Unaweza pitia maumivu Makali Sana yasiyofichika, lakini watu unaowaita wa karibu washindwe kuona hata tone la hayo maumivu, utatamani ukimbie dunia.
06. Wanaotupa support hawajawahi kutuacha, lakini ni watu wanaihitaji Sana support kama hiyo itokee kwao pia.
07. Kusahau wanaotusaidia wakati wa mapambano yetu, na kuwakumbatia watu from nowhere wakati wa mafanikio yetu.
08. Acha kupost wale unaowaona ni muhimu Sana kwako "my only one, my best, a friend to keep. My heart" .
Ni upumbavu Tu, maana watakaokusaidia ni wale ambao hata simu zao unapokea unapojisikia wewe.
Hao unaowaona wa muhimu Sana Ndiyo wataishia kukupa ahadi za uongo Tu.
Ndiyo maana mi sina marafiki kabisa.
09. Watu wanatekwa, wanapotezwa, wanauliwa lakini kuna watu wanajikuta hawaelewi kuhusu maumivu hayo yote. Wao ni kusifia muda wote upande unaohusika na Mambo hayo. Inasikitisha Sana, huwa najiuliza; je, hawa nao ni binadamu, na Sisi tunaoumizwa na hayo tupo kundi gani la viumbe hai kama hao wapuzi NAO ni binadamu? Maana hawawezi kuwa wenzetu katu, nakataa kuwa kundi moja pamoja nao.
##Kwa kweli inatafakarisha Sana