Inasikitisha sana kuona mbunge analalamikia wizi serikalini, Mwananchi wa kawaida analia

musase

Member
Jan 7, 2022
31
25
Sisi wananchi tunasikitika sana kuona Wabunge nao wanalalamika kuhusu wizi/ubadhilifu unaotekelezwa makusudi na watendaji wa serikali.

Kila mwaka mafuru yaleyale, bunge linalalamika bila kuchukua hatua watu wanaendelea, huku sisi mtaani shule zingine hazina walimu wa kutosha mpaka tunachanga kuajiri walimu, bima ya watoto wetu shida, madawa hivyo.

Kwa ujumla kuona bunge linalalamikia wezi badala ya kuchukua hatua thabiti, nashindwa kutofautisha mlalamikaji na mlalamikiwa.
 
Back
Top Bottom