Inasikitisha : Binti achinjwa kama kuku

Inasikitisha : Binti achinjwa kama kuku

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,369
Reaction score
27,787
Watu wasiojulikana wilayani Manyoni wamemchinja mithili ya kuku binti mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 16.

Diwani wa Kata ya Manyoni Mjini, Hamis
Masabuni alisema tukio hilo lilitokea juzi
asubuhi katika eneo la Mitoo kwenye
mashamba ya Magereza, Uwanja wa Ndege wa zamani. Alisema siku ya tukio, yeye alipata taarifa ya
simu kutoka kwa raia wema hivyo ikambidi aende huko kushuhudia kulikoni na mara alipofika eneo hilo alikuta mwili wa marehemu ukiwa umelala chini na kuchinjwa mithili ya
kuku.

Diwani huyo amelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo ili kubaini wauaji wa binti huyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao. Muuguzi wa zamu katika hospitali ya wilaya ya Manyoni, Getruda Njughuda amekiri kuupokea
mwili wa binti huyo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.


Chanzo : Habari Leo
 
nmh binadamu cc cjui tuna roho gan cku hz
 
May her soul R.I.P. Wahusika wa tukio hilo wanafaa kunyongwa endapo watabainika maana ni jambo la ukatili sana.
 
Kichwa chako kitakuwa kimejaa funza watupu, huwezi leta koment ya kijinga kwenye habari ya huzuni kama hii, hao wajinga wenzako wafuate hukohuko fesibuku. RIP BINT!

Mkuu watu kama hawa ni kuwapuuza tu, hawajui tofautisha furaha na huzuni.

Ni shidaaa.,.
 
Kichwa chako kitakuwa kimejaa funza watupu, huwezi leta koment ya kijinga kwenye habari ya huzuni kama hii, hao wajinga wenzako wafuate hukohuko fesibuku. RIP BINT!

Ukiongea point lazima nikupongeze. R.I.P
 
dah! nadhani mwisho wa Dunia u karibu kuliko tunavyodhani
 
Ndo tabu ya kula michemsho ya watu bure afu unakimbia
 
Back
Top Bottom