Serikali Iboreshe shule zake... Hizi feza na the likes hakuna kitu zinafanya zaidi ya kudidimiza hata kile kidogo tungeweza kusalvage kwa maslahi ya taifa na utamaduni wetu..
Piga marufuku mamitaala ya kingereza.. turudie kiswahili. Na Kiingereza kifundishwe tu kama lugha. Hata hivyo waliosoma chini ya utaratibu huu ndio wanaoongea na kuandika kiingereza na kiswahili sanifu.. hawa wa kisasa utopolo mtupu.
Na pia tuwaseme wanaouza heshima kama hao waliotoa maelekezo kwa dereva katika bandiko. Wazazi wengi tumeingia kwenye mtego wa mabeberu.
Tunajinyima kufika hatua ya kukufuru ili tu watoto waende kwenye shule zitakazo wafanya waheshimiwe...
Na sio waende kuelimika ili waheshimiwe kwa.mchango na maarifa waliyoyapata. Poleni kwa kusema mbali kabisa na bandiko..nimewiwa kusema hili kwa maana hata katika kazi kuna hii stigma.. haupimwi kwa uwezo ila kwa ufahari wa taasisi.
Ni aibu.. systematically tumeelimishwa vyetu ni vya hovyo.. na sasa tumehitimu maana tunafadhili muendelezo wa kudidimiza vya kwetu.. kwa fedha zetu wenyewe za ngama...
🙁
Sent from my Infinix X650 using
JamiiForums mobile app