sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
Inashangaza kusikia halmashauri fulani imepata hati safi wakati katika idara zake kuna wizi na ufisadi uliokithiri. Sekta za afya, elimu, miradi ya maendeleo unaona kabisa wizi uliotukuka halafu unakuja kusikia halmashauri imepata hati safi!!
Hati hizi husafishwa na kalamu siyo safi kweli. Majipu mengi madogo madogo ambayo ukiyaunganisha unapata jipu kubwa kuliko yanayotumbuliwa, yapo halmashauri na ndiyo chanzo cha migogoro kwenye ardhi, elimu, sekta ya afya, n.k.
Nitoe mifano michache: unakuta pesa imetengwa nyingi kwa ajili ya ujenzi w jengo fulani, lakini utakuta tu msingi wa muda mrefu ambao hauendani na gharama halisi, sekta ya manunuzi yapo manunuzi hewa na manunuzi ya gharama za juu kuliko gharama halisi, pia kuna manunuzi ambayo kitu kimenunuliwa lakini kimekufa baada ya muda mfupi. Mfano mwingine ni kughushi nyaraka mbalimbali kuwa mtumishi fulani kalipwa kiasi fulani na sahihi ipo ila mhusika hakupewa chochote na wala hajui hasa malipo ya likizo, night, kuna mkuu wangu wa idara alikuwa anaweza kucopy sahihi ya kila mwanaidara na anaenda kudai nayo malipo.
Both capital and revenue expenditure kwenye halmashauri nyingi wizi ni mkubwa, halafu unasikia halmashauri imepata hati safi! Barabara inaandikiwa kulimwa kwa kiwango cha Moram kilometre 10, barabar inavurugwavurugwa na kutengeneza mkondo mbaya wa maji yaharibu hiyo barabara zaidi ili bajeti ijayo wapate pesa nyingi zaidi pamoja na ya kuweka makalvati!
Wakaguzi wa mahesabu nao ni majipu yanayotakiwa kutumbuliwa either kwa kukosa sifa za kufanya kazi kwa umakini, ama kwa kupokea rushwa ili watoe hati safi wakati ni chafu.